Uzazi kwa operation

Uzazi kwa operation

khamsa

Senior Member
Joined
Jul 17, 2012
Posts
155
Reaction score
48
Naomba ushauri kwa wataalamu mana jambo linanitia hofu sana. ni kwamba mke wangu amejifungua kwa operation miezi sita iliyopita sasa tumegundua amepata mimba nyingine wakati afya yake haijatengamaa. Kuna athari gani kwa mama na mtoto?
 
We jamaa ni hatari, kaa mbali kabisa na mkeo na unahitaji kufuli la chuma.

Ndugu haijalishi kujifungua kwa oparation au kawaida, mtu aliejifungua miezi sita iliyopita hapaswi kuwa na mtoto mda huu, ilitakiwa mkae miaka miwili au mitatu ndo upachike nyingine.

Hapo unamuua/ kumkongorosha mkeo mapema aisee, nenda hospitali ukapate ushauri zaidi, au abort the mision.

Siku nyingine suala la mpango wa uzazi lizingatie sana na linawahusu wote wawili usimwachie mkeo peke yake maana kwa tukio hili linanipa picha kwamba mkeo anakuamini sana na mambo yako ila hapa umemwangusha sana na imani kwako itaanza kupungua, usimlaumu maana uzembe wako ndo unasababisha.
Tumia kondom hata kama hutaona utam.
 
Rudi kwa daktari wake aliemfanyia operation. Atawashauri cha kufanya. Ni ngumu sana kwa mwili wake ila anahitaji support kweli kweli.
 
hongera.....najua ulishindwa kuvumilia Ndio uanaume huo jamaa yangu . King'asti kakupa ushauri mzuri jaribu kuufutilia ......
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom