Uzazi wa mpango: Nafikiri ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kutupangia idadi ya watoto

Uzazi wa mpango: Nafikiri ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kutupangia idadi ya watoto

Wacha waendelee kufyatua vinginevyo panya Road watapungua mitaani. Rasilimali watu ya panya Road inategemea watu wanaozaa watoto hovyo hovyo na kushindwa kuwapa malezi.
 
China imeendelea kwa Kasi sana kwa sababu ya idadi kubwa ya watu.

Matajiri kibao ulaya na America walienda kufungua viwandani China kasababu ya cheap labor maana China mainland majobless walikua kibao.

Ukitangaza ajira Kwa ujira mdg
Majobless kibao china wataichangamkia
Ukienda sokoni unashusha Bei unauza mzgo haraka.

Ndo maana bidhaa za China duniani kote (hata zenye ubora sawa na za ulaya)
zinauzwaje Bei rahisi Sana sokoni kutokana na gharama ndogo sn za uzalishaji uko viwandani.

Sent using JamiiForums mobile app
 
Wacha waendelee kufyatua vinginevyo panya Road watapungua mitaani. Rasilimali watu ya panya Road inategemea watu wanaozaa watoto hovyo hovyo na kushindwa kuwapa malezi.
Suala la usalama wa raia na rate ya uhalifu havihusiani kabisa na kuzaa Sana mkuu.

Kwa taarifa yako,
Nchi yenye crime rate ndogo zaidi duniani Ni UAE, kwa waarabu ambako wanazaana Kama sisimizi.

Ila uko kwao wanalala milango wazi,
Viwango vya uhalifu Ni vidogo mno kulinganisha na nchi za south America na central europe Kama Italy kulikojaa mateja,wezi,majambazi na matapeli lukuki ya dunia hii.

Sent using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri ni wakati muafaka sasa kwa serikali kutupangia idadi ya watoto na siyo kuzaana zaana tu, tukiendelea na tabia hii, nchi itashishwa kujiendeleza na kufanya kazi ya kujenga mashule na mazahanati, lazima kuwe na limit, ili pesa inayopatikana ikafanye maendeleo mengine.
Mkuu, minafikiri unamawazo tegemezi, mipango mibovu na umasikini ndio tatizo kubwa linalo kuumiza.
Mimi nina watoto 8 na wote hakuna anaesoma shule ya serikali sijui mnaita elimu bure. Binafsi siamini kama elimu bora inaweza ikapatikana bure.
Kwaushauri tu, zaa watoto kulingana na uwezo wako na usije ukapanga kusaidiwa kulea ama kusomeshewa watoto wako kamwe.
 
Nchi kama tz inahitaji mipango thabiti hasa inshu za population control mana hii nchi wajinga wengi na wanazidi kuzaa wajinga tupu,china haikifika hapo ilipofika bila kuweka mikakati maalaumu juu ya population ya watu wake.
Upo sahihi mkuu.
Lakini mimi naamini kwamba, kama mzazi ni jukumu lako kuanza kuweka mioango thabiti kwa watoto wako hasa kwenye elimu, lishe, malazi na matibabu.
Sasa....
Niujinga ulio changamka kukuta mzazi anazaa watoto wake kwa kutegemea mipango ya serikali, na hapa ndipo mzazi yule anapo tengeneza another generation ya wajinga.
 
Acha ushamba
Watu Ni mtaji mkuu
Watu Ni nguvu Kazi ya taifa
Watu Ni jeshi la taifa
Watu Ni soko la ndani
Hakuna mtu atakubabaisha pa kuuza bidhaa yako, utauza soko la ndani maisha yataenda.
Unayajua maisha wanayo ishi watu vijijini?
 
Wacha waendelee kufyatua vinginevyo panya Road watapungua mitaani. Rasilimali watu ya panya Road inategemea watu wanaozaa watoto hovyo hovyo na kushindwa kuwapa malezi.
Upo sahihi kabisa, hao road panya ni matokeo ya kuzaa na kisha wazazi kushindwa kuwajibika vilivyo kwa watoto wao wakisingizia serikali na magimvi ya wazazi wenzao
 
Unayajua maisha wanayo ishi watu vijijini?
Kwakua tayari wanatambua kwamba maisha yao ni duni, basi ni wajibu wao kuamua wazae mtoto mmoja au wawili au wasizae kabisa.
Sidhani kama ni jukumu la serikali kumfunua mtu akili na kumwambia asizae kwasababu hana uwezo wa kuwalea. Huu naita ni ujinga unao ongeza kizazi cha wajinga wengi zaidi
 
Ni kweli mkuu,ila kumbuka hao watu hawana Ufahamu wa mambo mengi..ndo maana kuna umuhimu wa serikali kuwapa hata elimu kuhusu umuhimu wa kuzaa watoto wachache ili waweze kuwamudu.
 
Ndugu Zangu Zaeni Elimu Ni Bure Hata India Na China Zimeendelea Sana Kwa Kuzaliana
Wewe Waziri Wa Afya Kwenye Utawala Wangu Sitaki Kusikia Kupanga Uzazi
Ngoja Nimalize Kipindi Changu Ndiyo Atakayekuja Mpange Uzazi

Kule Sijui Nchi Gani Wamebaki Wazee Watupu
Tuchape Kazi Tule Tushibe, Unajua Ndugu Zangu Usipokula Ukashiba Hata Uzazi Utagoma
Wale Wavivu Wanaogojea Mnazi Mmoja Hao Ndiyo Wafikirie Kupanga Uzazi

By Mzilankende Mnyago, Jiwe, Chuma,
 
Back
Top Bottom