Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima kwenu wanajamvi,
Leo Rais wetu Mheshimiwa Samia katutangazia matokeo ya sensa ya watu na makazi.
Ukiitazama vizuri idadi ya watu inavyoongezeka (61 million) na ukuaji wa uchumi ni wazi sasa tunatakiwa kuzalisha zaidi bidhaa mbali mbali kuliko kuzalisha watoto ambao watakuja kuangukia katika lindi la umaskini.
Tuzae watoto ambao tutakuwa na uwezo wa kuwatunza na kuwajengea misingi bora ya elimu.
Ni vyema familia zikapanga uzazi wa mpango ambao utaendana na uwezo wa uchumi na malezi bora.
Ongezeko la idadi ya watu bila ya ukuaji wa uchumi, maendeleo ya sayansi na teknolojia, matokeo yake ni kutengeneza kizazi cha madereva wa boda boda, wauza bar, machinga na wapiga debe.
Naomba kuwasilisha kwa mjadala wenye afya.