Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Ajira hamn mtu anachagua aisee! Mitaji ndio ishu huko kulima ambako hujui unamuuzia nani nalo ni swala jingine!Tanzania tuna tatizo la kuchagua ajira Tuna ardhi ya kutosha watu hawataki kulima na kufuga
Unalima kwa nguvu ukifika sokoni mmakuta wakulima mmejazana mazao hayana faida! Kama ni mali kuoza unauza kwa hasara tu ili kiishe.
Nani atafurahia kilimo cha aina hio? Raha ya kulima upeleke mazao sehemu husika ukabidhiwe chako mapema uendelee na mishe zingine! Peleka mazao ghalani gunia zako 10 unalipwa cash yako yenye faida nzuri unatembea.
Hiki kilimo cha kuanza kuviziana masokoni na madalali hakina maana wala tija! Uteseke kulima halafu ukifika sokoni dalali anataka ale 40% ya faida wewe uliyeteseka uambulie 60%! Hapo bado hujadhulumiwa!
System ya kilimo ki bongobongo haiko stable wenzetu wa Kenya wamejitahidi ku brand produce zao duniani wanauza direct ulaya huko! Wanakuja kulangua kwetu kwa bei nafuu wao wanauza kwa super profits ulaya!
Wamewezaje kushawishi wazungu wanunue bidhaa zao sisi tunashindwa nini ku standardize kilimo chetu kiwe cha kibiashara? Arable land ipo ila watu hawana time na kilimo sababu kinazalisha hasara kwa watu wasio na mitaji! Serikali inachoweza ni kutumia billion 27 kujenga AC za mtaani dodoma eti hali ya hewa ku maintain!
Mara elfu uwe mchuuzi wa mazao ila sio kilimo bongo kama huna mtaji wa maana!