Uzazi wa mpango ni suluhu ya matatizo mengi ikiwemo umachinga uliokithiri

Ukizaa wawili au mmoja unakuwa katika nafasi nzuri ya kufanya saving ya maana ambayo unaweza kuiwekeza na/au kuja kuwasaidia baadaye kama watahitaji msaada wako. Ukiwa na watano huwezi kufanya saving yoyote ya maana, kila utakachokipata itakuwa kwa ajili ya kuwalisha tu, hata mavazi au makazi bora itakuwa vigumu kuwapatia na baadaye wakija kutaka msaada wowote kwako hutaweza kuwapatia na badala yake wewe ndiye una uwezekano mkubwa wa kugeuka mzigo tena kwao wakiwa na haso zao.
 
Unazungumzia familia za wanaojiweza, na hawa mostly huwa na channels za connection kwa ajili ya ajira za watoto wao tena regardless ya idadi ya watoto walionao, vipi yule mama anaeuza vitumbua kumsomesha kijana wake mpaka chuo kikuu kwa msaada wa mkopo wa serikali, huyu atatoa wapi hiyo saving?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna watu walimuamini na wakafyatua kweri kweri!
Jiwe Watu Walimuamini Ataishi Milele Watu Wamezaa Mpaka
Mabadiliko Ndiyo Sasa Hivi Yaani Hatuamini Kinachokuja
Kupangwa Na Amos Makalla Na Mikoa Mingine Iki~Copy Kinachoendelea Dar Es Salaam


Mtu Mmoja Alimaliza Singida Fani Ya Records Management
Alipoona Hapati Kazi Akachukua Ushauri Wa Jiwe Azae
Ili Iwe Grease Yaani Milango Ya Ridhiki Ifunguke
Sasa Hivi Imekaza Milango Yote
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ameongelea changamoto za wakati uliopo,changamoto za mzazi wa miaka ya 70s au 80s ni tofauti na za mzazi wa miaka ya sasa kiufupi mambo mengi yamebadilika.maisha ya sasa kama huna kipato cha kutosha ,watoto wa tano au sita ni mzigo mzito,ajira hakuna na changamoto nyingi kiuchumi.
Ukiwa na watoto wawili unaweza kuwapambania kwa urahisi kuwatengenezea future kuliko kuwaacha wauze pipi na leso stendi.
 
Mkuu umeifupisha vizuri sana[emoji120].
Jambo hili lilipaswa kuwa common sense tu lakini haiko hivyo kwa wingi, inasikitisha sana.
 
ili uwe na watoto wenye future nzuri lazma nawe uwe na future nzuri kwanza!......nakusalimia sana mkuuu
Hii pointi imenifanya nijitazame mara mbili kama ninakidhi vigezo[emoji2][emoji2],kipande kifupi cha maneno yenye uzito mkubwa.
Kwa maisha yalivyo sasa wazazi tuna jukumu la kuwatengenezea njia watoto ,ukiachana na hilo la kuwapatia elimu bora.inabidi mzazi " uchungulie mbele namna gani watoto watadondokea sehemu salama."
 
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Wapate Elimu Nzuri, Tabia Njema, Connection Safi
It's Begin With You!!
 
Usifananishe majira ya babu zetu na haya majira ya sasa, ambayo sehemu ambazo yalikuwa mashamba imekuwa miji,nadhani umenielewa
 
Future nzuri ipi? Hao waliokuwa wakizaliwa dazani moja si ndio hawa machinga na bodaboda sasa hivi?
 
Ni kweli wazee wetu walikuwa hawazingatii uzazi wa mpango lakini tofauti na sisi ni kwamba mtoto akimaliza darasa la saba anakabidhiwa shamba lake mambo yanaenda, sasa hawa wa sasa wanakimbia Kijijini kuja mjini, na wanaomaliza chuo kikuuu nao wanataka lazima waajiriiwe, tena serikalini.
 
Kuna mahali nimesema watoto wauwae?
Hiyo misemo ya kila mtoto anakuja na sahani yake ni potofu, haina ukweli wowote wala nafasi katika dunia ya leo. Watoto wanatikiwa wakute sahani zao zilizoandaliwa tayari na wanaowazaa.
Unajua maana ya uzazi wa mpango?
 
Aisee Mimi nafikiri uzazi wa mpango sio suluhisho.Watu ni raslimali kama zilivyo raslimali nyingine. Hivi unajua pale kijijini mzee mwenye watoto 9 no tajiri kuliko yule mwenye motto mmoja? China kwa mfano INA watu wengi lakini haijatetereka ki uchumi.Inasemekana kuwa Tanzania ilipopata Uhuru thamani ya fedha za Tanzania na China zikilinganishwa na Dollar ya Marekani zilikuwa Sawa. Taratibu China ilianza kuiacha TZ huku idadi yake ya watu ikiongezeka.Leo hii uchumi wa China uko juu kwa TZ ni kama kichuguu na mlima Kilimanjaro.
Gharama ya kusomesha mtoto mwenye Shule za kiwango FORM ONE HADI CHUO KIKUU in mamilioni (mtaji) kijana akimaliza tayari uchumi wa familia umeshayumba wanatembelea miguu na mikono! Wakati huo kijana anazurura na mibahasha! bila ajira.
USHAURI!
Japo mtaniona mburula napendekeza Tanzania isimamishe zoezi LA kuandaa wataalamu wa hali ya juu ambao wanakuwa ma jobless mtaani hadi hapo kutakapokuwa na uhitaji kwani hata hawa waliopo hawajaweza kubadilisha uchumi wa Tanzania wengi wanakimbilia mwenye Siasa!
Badala take hizo fedha zitumike kuwaandaa RAIA vijana kwenye ufundi baada ya kumaliza elimu ya kati..OVA!
 
Na suluhu ya mashamba yasio na watu wakuyalima ni ipi? Wote wamehamia mjini wameacha wazee wasio na nguvu ndio walime, suluhu ni ipi?
Kuendeleza na kuimarisha mnyororo wa thamani katika kilimo.hii itasaidia kumpunguzia mkulima baadhi ya mizigo na kunufaika na kilimo kwa hali ya juu.

Baada ya hayo yote kwisha kufanyika vijana watarudi shambani kwa kasi wakiamini kua mali inapatikana shambani.
 
Maana ya uzazi wa mpango ni kupanga uzazi. Utaamua mwenyewe kama utumie kalenda, condom, vidonge, njiti, umwage nje, ukatwe n.k
Unajua maana ya uzazi wa mpango?
 
Wamachinga wengi wanalalamika wana watoto wa kuwalisha hivyo wasiondolewe kwenye maeneo yao ya sasa !
 
Tatizo linaloikumba Hifadhi ya Ngorongoro kwa sasa ni ongezeko kubwa la Idadi ya watu. Kadri idadi ya watu inavyozidi kuongezeka ndivyo uharibifu mkubwa wa mazingira unavyoongezeka na inapelekea kuongezeka kwa hali ngumu zaidi ya maisha kwa watu walio wengi.
 
Kwenye Utawala Wangu Ndugu Zangu Zaeni
Kama Unategemea Mnazi Mmoja Ndiyo Ufikirie Kupanga Uzazi
Tena Uzazi Utagoma. Nayasema Haya Na Waziri Wa Afya Yupo Hapa
By Mzilankende Mnyago
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…