Uzazi wa mpango

Bhudagala

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2014
Posts
325
Reaction score
311
Habari wakuu!
Nimeamua uzi huu kuupa kichwa hicho, naomba kuuliza kwamba. Mwanamke baada ya kujifungua huchukua muda gani kuanza kuona siku zake? Na Je, akifanya tendo la ndoa ndani ya miezi miwili baada ya kujifungua inaweza kupelekea kubeba ujauzito ilihali hata siku zake hajaziona?
Asante!
 
Kwema.

Kwanza, baada ya kujifunga mara nyingi huchelewa kuona siku zake (wengine hupitisha hata zaidi ya miezi mitano), urefu wa kipindi cha kutoona siku hutofautiana baina ya mwanamke na mwanamke.

Hili sio tatizo ila ni namna ya mwili kurudi katika hali yake ya kawaida (normal physiology).

Licha yakua mwanamke kutoona siku zake mara tu baada ya kujifungua sio tatizo hii pia ni NJIA YA UZAZI WA MPANGO kwa njia za asili (natural methods) kwa kitaalam inifahamika kama Lactational Amenorrhea, kwenye kipindi hiki mwanamke anapokua ananyonyesha.

Hivyo basi ili njia hii ya uzazi iweze kufanya kazi kwa kiwango kikubwa mwanamke anatakiwa kufuata taratibu fulani za kitaalam ikiwa ni pamoja na Kumyonyesha mtoto maziwa tu bila kuchanganya na vyakula vingine.

Asante na Karibu.
 
Asante sana
 
Siku mke wangu akizaa nitarudi kusoma huu uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…