Habari wakuu natumaini muko vizuri.
Maisha yangu yanaendelea kunishangaza kila siku kuhusu nyakati zangu, Nimekuwa nikiishi kama kijana mdogo wa kawaida lakini kumbe jamii hainioni kuwa ni kijana mdogo bali inaniona ni Mtu anaefukuzia uzee.
Nilizoea kupewa shkamoo na watoto wadogo lakini sasa napewa shkamoo na vijana wakubwa tuu ambao Mimi nilihisi pengine tuko sawa. Mwanzo walikuwa ni vijana wakubwa wachache lakini saizi ni vijana wengi sana wakubwa wananipa shkamoo, wengine wananiita baba kabisa.
Siku Moja ndio nilishangaa kabisa pale nilipotaka kujipatia kamchepuko majibu yake yakaniacho hoi "kalisema lakini wewe mbona kama baba yangu tuu "
Uzee umepiga hodi kwenye maisha yangu na Bado hata sikujipanga vizuri kuupokea.
NB: MWENZAKO AKINYOLEWA ZAKO TIA MAJI