Hivi ukishushia Mombasa taratibu zinakuwaje? Kule unalipa nini? Na TZ unakuja kulipa nini? Maana isije mtu ukalipishwa Mara 2!Bora tuwapatie mapato mombasa port
Ivi serikali inaona jinsi inavyopoteza mapato. Naona kama tunaibiwa fedha zetu unalipia mzigo kodi zote lakini mzigo wako unashikiliwa hupewi Ati system hazifanyi kazi kibaya zaidi unazidi kulipishwa port charges. Hii ni aibu na hatutaweza kujikwamua kiuchumi. Aibu sana kwa nchi yetu
Kama tatizo lipo system za TRA sema, kama liko system za bandari pia SEMA, usijeneralaiz mambo. Tatizo clearing agent wengi wanajuwa tatizo liko wapi, wanababaisha tu wateja.
huu ni ujinga na upumbavu kabisa unaofanywa na wausika wa bandari. nawashauri wafanya biashara wenzangu, hakuna haja ya kuikimbia bandari yetu ya apa dar kwenda mombasa, ni haki yetu kuitumia, mizengwe wanayo ileta tutawaanika mpaka hata bungeni. siyo nyie mnaendelea kuota vitambi kama nundu la ngamia sisi uku tunakonda kwa kukwamisha mizigo yetu. tutachachamaa mpaka hivyo vinundu vyenu (vitambi) vitayeyuka. jirekebisheni mbona kupokea hela hamsemagi system mbovu. mabwege kweli kweli na hamna hadabu.