UZEMBE:NAMUNGO VS MBEYA KWANZA KUHAIRISHWA

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
5,794
Reaction score
5,352
inawezekana vp manispaaa ina gari moja tu la wagonjwa... inakosa ambulesi katika mechi muhimu kama hii

Au ni hujuma tu ili mbeya kwanza wapate ponti za bure

Mechi kuhairishwa kwa sababu ya kutokuwepo gari ya wagonjwa ni sheria ya kipuuzi..gari lilipata dharula ya kupeleka mgonjwa mechi si ingeendeleea tu maana gari lingerudi..kuliko kuhairisha kabisa
 
Kabla ya gari kurudi Kwa mfano mchezaji angepata majeraha ya kupelekwa hospital haraka iwezekanavyo wangetumia usafiri Gani kwenda hospital kunusuru maisha ya mchezaji?
 
Ambulance ni muhimu kuwepo uwanjani, ni bora walivyozingatia sheria, health and safety ya wachezaji wakiwa uwanjani ni muhimu sana
 
Kabla ya gari kurudi Kwa mfano mchezaji angepata majeraha ya kupelekwa hospital haraka iwezekanavyo wangetumia usafiri Gani kwenda hospital kunusuru maisha ya mchezaji?
Mfano mchezaji akipata majeraha na kupelekwa hospitali.. Je..? Mechezo utaghairishwa.

Maana uwanjani hapatokuwa na gari ya wagonjwa tena.

Au kuna backup..? Kama kuna backup kwanini isitumike now..?

Au mchezo utasimama hadi gari itakapo rejea..?

Au gari lililopata dharura limepeleka mgonjwa KIGOMA..?
 

Hoja yako inamantiki, lakini Naona walioahilisha wameangalia Sheria inasemaje, kama Sheria inasema mpira kabla ya kuanza NI lazima iwepo gari ya wagonjwa basi wapo Sawa.

Tufuate Sheria , hakika kama game ingechezwa na lingetokea la kutokea yangesemwa mengi zaidi ya haya.

Tufuate Sheria tulizojiwekea
 
GAME HAIJAAHIRISHWA...
hapo Mbeya Kwanza wapewe points zao..
Ndio kanuni inavyosema..
Maana ukisema imeahirishwa maana yake itachezwa Tena
 
Nakumbuka msimu uliopita ruvu shooting hawakupeleka ambulance uwanjani pale mabatini, walipokwa point
 
Watacheza hata siku nyingine sio lazima leo, hamna point za bure
 
Tatizo la waafrika tumezoea kupeleka mambo kibishibishi sa ikitokea mtu akafaint uwanjan atapelekwaje hospital
 
Tatizo la waafrika tumezoea kupeleka mambo kibishibishi sa ikitokea mtu akafaint uwanjan atapelekwaje hospital
Sawa ...what if mtu amefaint uwanjani na gari ikampeleka hospital..mechi inasimama mpaka gari lirudi????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…