Uzembe wa Madaktari: Msaada wa kisheria unahitajika haraka

Uzembe wa Madaktari: Msaada wa kisheria unahitajika haraka

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
20,834
Reaction score
26,217
Habari WanaJF

Kuna huyu ndugu yangu amepata matatizo, kama kuna mwenye kujua namna ya kumsaidia apate msaada wa haraka nitashukuru.

Kisa chenyewe ndiyo hiki;

Jamani ndugu zangu matatizo yamezidi kuniandama tena, la mtoto limepita limekuja tena la mama watoto baada ya mke wangu kuzalishwa pale Sinza Palestina mtoto kwenda kufia Mwananyamala hospitali. Usiku huu wa J2 kuamkia J3 nipo hospitali ya Mbezi baada ya mke wangu kupata maumivu makali ya tumbo usiku huu kafanyiwa uchunguzi kumeonekana bonge la pamba tumboni imeachwa eidha kwa makusudi au kwa uzembe.

Kwanini nisiseme hata mtoto alikufa kwa uzembe wa hao hao? Ninachoomba ni msaada wa kisheria, nina imani huku tupo watu tofauti tofauti.

Namba yangu ni 0715724897 au 0767624897 naombeni msaada wenu!

Tumsaidie apate haki yake mbali na kwamba alishapoteza mtoto.....

Natanguliza Shukrani kwenu!!
 
Poleni sana kwa matatizo, natumaini wanasheria watakupa msaada mkuu
 
Poleni sana.

Ni matumaini yangu kuwa JF kuna wanasheria na wasomi wa sheria wengi tu wanaoweza kuwapa ushauri wa nini cha kufanya.
 
Kifo cha mtoto kilisababishwa na nini? Alionekana kuwa kuna ugonjwa wowote uliomsababishia kifo chake? Death certificate imeandikwa sababu ya kifo cha mtoto ni nini? Tuanze na hayo kwanza
 
Kifo cha mtoto kilisababishwa na nini? Alionekana kuwa kuna ugonjwa wowote uliomsababishia kifo chake? Death certificate imeandikwa sababu ya kifo cha mtoto ni nini? Tuanze na hayo kwanza

mkuu mtoto alizaliwa kabla ya wakati i mean akiwa na miezi 7 mbali na hilo manesi walifanya uzembe mkubwa kwa kuchelewa kumzalisha mama baada ya kusukuma kwa muda mrefu na matokeo yake mtoto kunywa maji ya placenta yaani amniotic fluid ndipo hapo akahamishiwa Mwananyamala alipofia, hana death certificate ya mtoto.


karibu kwa ufafanuzi zaidi..
 
Dah!Poleni sana!Inatia Uchungu na Hasira kwa Uzembe kama huo.Moja ya mambo ya kufanya kwa sasa ni kupata report zote za madaktari juu ya sababu za Kifo cha mtoto, na pia tukio la mwisho la kukutwa na pamba ndani.Report ieleze madhara aliyopata victim.Pamoja na kuwepo kwa Disciplinary Body ya Madaktari,lakini Uzembe huu si wa kuachwa hivihivi bila Adhabu.Sheria ya Madhara Inachukua Nafasi hapa.Ila kikubwa kwa sasa tulia na kumuhudumia mgonjwa.
 
Nenda pale kijitonyama, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wanaweza kukusaidia.
 
Kaka pole sana na matatizo hayo, hapa niwazi kwamba ni uzembe wa madaktari ila cha msingi maliza kumhudumia mgonjwa kwanza,chukua reports zote za daktari akisha pona nenda kijitonyama krb na chuo cha ustawi wa jamii ukawaone wale kituo cha sheria na haki za binadamu utapata msaada na haki itapatikana
 
Ushauri wangu nenda kaonane na wanasheria phisicslly hilo swala lako linahitaji umakini Sana, nahapo unaweza kuishitaki jospitali km hospitali kwa sababu dokta kaajiliwa na serikali inana nawanasheria km huyo mama kapata madhala kutokana na hiyo pamba
 
Kibongobongo wagonjwa wengi sana tunapona kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu na si kwa uwezo wa kitaalam wa Madaktari wetu,wataalam wetu wa Utabibu wengi wao japo si wote ni Mazafantaz sana
 
Back
Top Bottom