Uzembe wa SADC kuligeuza jeshi lake liwe la kulinda amani DRC badala ya kupigana ndicho kinachofanya M23 na Rwanda waonekane kama wana uwezo mkubwa

Jamiitrailer

Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
80
Reaction score
208
Jumuiya ya SADC inafanya maamuzi kiwepesi na kutekeleza maazimio yake ya kuilinda Congo DRC kwa mtindo wa kizimamoto.

Mwezi Mei 2023,SADC ilipitisha azimio la kupeleka jeshi lake Congo DRC,ambayo ni nchi mwanachama ili kusaidia kurudisha hali ya amani eneo la mashariki DRC.

Jeshi la SADC lilopelekwa sehemu ni kikosi kutoka South Africa,lakini kuna vikosi vya Malawi na Tanzania pia.

Msingi wa kisheria wa SADC kupeleka jeshi lake DRC uko katika mkataba wa makubaliano ya nchi wanachama ya mwaka 2003 yanayoainisha kwamba shambulio lolote kwa nchi mwanachama litatafsiriwa kama kitisho cha amani na usalama kwa nchi zote wanachama,na hivyo nchi zote zitashirikiana kuzima tishio hicho.

Kikosi cha SADC kilipewa jukumu la kuisaidia serikali ya DRC katika kurejesha amani na utulivu kwa kuisaidia kijeshi katika mapigano dhidi ya waasi na kunyang'anya silaha zao....,kwa maana nyingine siyo kikosi cha kulinda amani( peace keeping mission) kama vikosi vya UN ambavyo hukaa katikati ya mahasimu ili wasipigane.

Uzembe wa viongozi na watunga sera wa SADC ni kwamba,pamoja na kuvijua kwao kiundani vikosi vya waasi vilivyomo DRC,ikiwa ni pamoja na M23 na namna wanavyosaidiwa na Rwanda..na aina ya silaha walizonazo, ..lakini bado wakalifanya jeshi la SADC liingie DRC kama kulinda amani tu na siyo kimapigano.

Mathalan, walikubaliana kikosi cha wanajeshi 5000 kipelekwe kwa kuanzia,lakini wamepeleka askari 1300 tu wenye silaha za kulindia amani zaidi kuliko za mapigano kisasa katika uwanja wa vita.
Kichekesho ni kwamba wanajua idadi ya kikosi cha adui anazidi chao....,na wanajua pia aina ya silaha aliyonayo adui wanayekwenda kumkabili. Ni kama kuamua kwenda na mishale vitani,wakati unajua adui ana bunduki.

Kana kwamba haitoshi,kikosi cha SADC kinakosa hata kuwa na surveillance drones ...vifaa muhimu kwa jeshi la ardhini kwa sasa ambazo zingewawezesha kuona vikosi vya M23 vikifanya approach hapo mjini siku waliyoshambiliwa. Hata jeshi chovu la UN wanazo drones,japo kikosi chao hakipigani.

Ikumbukwe kuwa kikosi cha Umoja wa Africa(AU) ambacho kilihusisha pia Tanzania ,kilichokwenda DRC mwaka 2013 kwa lengo la kuwapiga waasi wa M23 kilijipanga kwa kazi hiyo...,na matokeo yake waasi wakapigwa na kukimbilia kwao Rwanda na Uganda.
Jeshi la SADC limepelekwa kama linaenda kupatanisha kati ya wagomvi wawili.

Watengeneza sera wa SADC waliweka siasa katika kutekeleza masuala ya kiufundi ya kijeshi kutokana na ubahili.
 
watutsi tuko vizuriii mazeee dah tumejipangaa yaani adi rahaa....kipigo tunachokitoa apo congo sio cha karne hiii...jeshi la wazee tz libaki kilio na kwikwi..mkongomani atulie na ndombolo yakee...next tunauteka mji wa bukavuu na mbuyi mayii
 
Kiufundi, SADC haipaswi kuwa na chombo cha kijeshi.

SADC ni kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi kwa nchi za kusini mwa Afrika. Chombo kinopaswa kuunda jeshi moja lenye nguvu Afrika ni Umoja wa Afrika AU pekee.

Hilo litakuwa jeshi imara na lenye vituo Katika kanda zote za Afrika Mashariki, Kusini, Magharibi, Kaskazini.

SADC haina uwezo wa kifedha kuweza kuwa na jeshi imara la kuweza kukabiliana na changamoto kama migogoro ya kijeshi kwa upande huo.

Tuliona mfano (kama wafahamu) raisi Nyusi aliomba msaada wa kijeshi ili kukabiliana na wale magaidi kule Delgado Msumbiji na SADC ilishindwa kazi hiyo.

Ni pale walipoiomba Rwanda ambayo ipo nje ya SADC isaidie na kulipofikiwa makubaliano kati ya Rwanda na SADC na Msumbiji ndo Rwanda ikaingiza jeshi lake la kisasa nchini Msumbiji na hadi leo kumetulia.

Sasa weye fikiria nchi 16 za SADC hazina uwezo wa kijeshi wa kuisaidia nchi mwanachama ya Msumbiji kukabiliana na magaidi walokuwa wakitishia usalama wa eneo la kusini.
 
Samahani, wewe ulijua vipi kama hawana?? Ulikuwepo eneo la tukio??
Mkuu Enzo...,katika masuala haya majeshi yanayokwenda katika missions kama SADC,UN na AU hakuna siri. Kwa mfano jeshi la kulinda amani wanazo drones. Hakuna siri pia kwamba kuna wakati Rwanda walikuwa wakifanya jamming drones pilots wasome WRONG READING ili location halisi ya M23 iionekane tofauti...lakini kuitegua hiyo ni mchezo mdogo tu. Na siyo siri pia idadi kamili ya kikosi cha M23 na wanajeshi wa Rwanda wanaosaidia,na aina ya silaha walizonazo pia hakuna siri .
Ndo maana nasema ni uzembe wa SADC kulipeleka jeshi kana kwamba linaenda kulinda amani wakati linakwenda katika actual combat
 
Kwa hiyo sie tuwekeze afu tuwachekee mkiharibu sio
 
katika masuala haya majeshi yanayokwenda katika missions kama SADC,UN na AU hakuna siri.
Nani alikuambia kuwa hakuna siri?? Drones kwako ni kitu kikubwa kumiliki?? M23 wawe na drones halafu UN wasiwe nazo??
 
Mwanzo, malengo na maona ya SDC yalikuwa kuhusu kukuza ucumi na ushirikiano kibiashara pekee....,lakini mwaka 2003,wakaongeza articles katika katiba yao zilizohusu jumuia kubeba jukumu la kiulinzi na kiusalama kwa nchi wanachama....article inayosema kushambuliwa kwa nchi moja mwanachama kutatafsiriwa kama shambulio na tishio kwa nchi zote katika jumuiya,..hivyo basi jumuiya itakuwa na jukumu la kuzima tishio hilo kwa pamoja.
Lakini kama ulivyosema ni wagumu kuweka commitment ya kifedha katika kutekeleza malengo yao. Na kama ni hivyo basi, ni bora waache kupeleka vikosi vyao katika maeneo ya vita kuliko kupeleka kikosi kinachokwenda kupigana lakini umewapa nyenzo zisizoendana na mahitaji ya combat.
Wataalam wa masuala ya ulinzi wa SADC walihitaji kikosi cha watu 5000 na aina fulani ya vifaa hiyo siyo siri ...lakini watunga sera wakapeleka askari 1300 tu na vifaa duni kabisa
 
We kubali mmechezea kichapo tantalila nyingi za nini unaenda kulinda amani umeambiwa m23 wanaitaka amani
 
Nani alikuambia kuwa hakuna siri?? Drones kwako ni kitu kikubwa kumiliki?? M23 wawe na drones halafu UN wasiwe nazo??
Umeona?
Hakuna siri kweli..na hata M23 wanazo drones..na wana jamming devices za kufanya manipulation ya location. Na siyo siri aina ya siri walizonazo ukubwa wa kikosi chao. Lakini hapa nazungumzia mapungufu na uzembe wa kikosi cha SADC..kwamba wanajua hayo yote lakini bado wakapeleka kikosi kidogo sana na chenye vifaa hafifu lana kwamba jeshi lao linakwenda katika peace keeping mission...,na ukweli ni kwamba wako katika peace keeping mode..ndo maaana walikamatwa wakiwa odd guard kirahisi
 
We kubali mmechezea kichapo tantalila nyingi za nini unaenda kulinda amani umeambiwa m23 wanaitaka amani
Nimesema wamepigwa..,lakini wamepigwaje?
Nilichotaka kusema hapa ni kwamba mara nyingi wanajeshi wa Tanzania wakiuawa katika mission za majeshi ya pamoja iwe majeshi ya UN,AU, East Africa au SADC ...inakuwa katika mtindo wa namna hii..wanapelekwa kulinda amani..jeshi ambalo linafanya kikosi kisishambulie....,kiwe cha kujihamia tu. Na hali hiyo ndo ilimfanya rais Tsitshekedi kuamuru majeshi ya East Africa na UN yaondoke tu maana hayajihusishi katika mapigano halisi.
Lakini
wamspeleka jeshi kisiasa bila mahitaji yaliyoorodheshwa na wapiganaji wenyewe,...walifikiria nini?
 
Wewe kichapo ni kichapo tu
 
Wewe kichapo ni kichapo tu
Kuna kichapo cha kujitakia na kichapo cha uzembe.
Ni sawa na kuingia katika uchaguzi wakati unajua atakayehusika kuratibu kura ni mkwe wa mshindani wako....,matokeo yakija mpinzani wako lashinda kwa 99.9% usilete lawama
 
Kwanini Sadc wampiganie DRC, yeye hana jeshi? Hana silaha? Hana mbinu? Si ni nchi huru?
 
hata UN hawana jeshi la kupambana ni hivyo hivyo tu wanaishia kupatanisha kwa mdomo tu na kulaani kwa maneno tu
 
Kuna kichapo cha kujitakia na kichapo cha uzembe.
Ni sawa na kuingia katika uchaguzi wakati unajua atakayehusika kuratibu kura ni mkwe wa mshindani wako....,matokeo yakija mpinzani wako lashinda kwa 99.9% usilete lawama
Ushachezea uguza manundu yaani ma nchi kibao mmeungana muwachangiz m23 mnaakili timamu kweli
 
Hata zikienda nchi zote kupigana huko mambo hayatakuwa rahisi kama unavyofikiria.
 
Nyuzi karibia ya Tatu hii leo JF ikiwadogosha Jeshi letu kiaina.

batu ba
meshapata vinusu taarifa huko wanapika na kusambaza haya madudu. Mola yanje.

Hizi ndizo propaganda zenyewe.

Sikilizeni, waleteni tu hao wazungu waje wachukue hizo mali, kwani mali zenyewe zishakuwa cursed. Vifo kila musehemu. Gamna sababu za kuleta hizi propaganda tunyooshe mikono halafu tiseme Balete.

Njooni tyu, mbona mpo huko? hizi kampeni mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…