Jamiitrailer
Member
- Oct 20, 2019
- 80
- 208
Jumuiya ya SADC inafanya maamuzi kiwepesi na kutekeleza maazimio yake ya kuilinda Congo DRC kwa mtindo wa kizimamoto.
Mwezi Mei 2023,SADC ilipitisha azimio la kupeleka jeshi lake Congo DRC,ambayo ni nchi mwanachama ili kusaidia kurudisha hali ya amani eneo la mashariki DRC.
Jeshi la SADC lilopelekwa sehemu ni kikosi kutoka South Africa,lakini kuna vikosi vya Malawi na Tanzania pia.
Msingi wa kisheria wa SADC kupeleka jeshi lake DRC uko katika mkataba wa makubaliano ya nchi wanachama ya mwaka 2003 yanayoainisha kwamba shambulio lolote kwa nchi mwanachama litatafsiriwa kama kitisho cha amani na usalama kwa nchi zote wanachama,na hivyo nchi zote zitashirikiana kuzima tishio hicho.
Kikosi cha SADC kilipewa jukumu la kuisaidia serikali ya DRC katika kurejesha amani na utulivu kwa kuisaidia kijeshi katika mapigano dhidi ya waasi na kunyang'anya silaha zao....,kwa maana nyingine siyo kikosi cha kulinda amani( peace keeping mission) kama vikosi vya UN ambavyo hukaa katikati ya mahasimu ili wasipigane.
Uzembe wa viongozi na watunga sera wa SADC ni kwamba,pamoja na kuvijua kwao kiundani vikosi vya waasi vilivyomo DRC,ikiwa ni pamoja na M23 na namna wanavyosaidiwa na Rwanda..na aina ya silaha walizonazo, ..lakini bado wakalifanya jeshi la SADC liingie DRC kama kulinda amani tu na siyo kimapigano.
Mathalan, walikubaliana kikosi cha wanajeshi 5000 kipelekwe kwa kuanzia,lakini wamepeleka askari 1300 tu wenye silaha za kulindia amani zaidi kuliko za mapigano kisasa katika uwanja wa vita.
Kichekesho ni kwamba wanajua idadi ya kikosi cha adui anazidi chao....,na wanajua pia aina ya silaha aliyonayo adui wanayekwenda kumkabili. Ni kama kuamua kwenda na mishale vitani,wakati unajua adui ana bunduki.
Kana kwamba haitoshi,kikosi cha SADC kinakosa hata kuwa na surveillance drones ...vifaa muhimu kwa jeshi la ardhini kwa sasa ambazo zingewawezesha kuona vikosi vya M23 vikifanya approach hapo mjini siku waliyoshambiliwa. Hata jeshi chovu la UN wanazo drones,japo kikosi chao hakipigani.
Ikumbukwe kuwa kikosi cha Umoja wa Africa(AU) ambacho kilihusisha pia Tanzania ,kilichokwenda DRC mwaka 2013 kwa lengo la kuwapiga waasi wa M23 kilijipanga kwa kazi hiyo...,na matokeo yake waasi wakapigwa na kukimbilia kwao Rwanda na Uganda.
Jeshi la SADC limepelekwa kama linaenda kupatanisha kati ya wagomvi wawili.
Watengeneza sera wa SADC waliweka siasa katika kutekeleza masuala ya kiufundi ya kijeshi kutokana na ubahili.