Jumuiya ya SADC inafanya maamuzi kiwepesi na kutekeleza maazimio yake ya kuilinda Congo DRC kwa mtindo wa kizimamoto.
Mwezi Mei 2023,SADC ilipitisha azimio la kupeleka jeshi lake Congo DRC,ambayo ni nchi mwanachama ili kusaidia kurudisha hali ya amani eneo la mashariki DRC.
Jeshi la SADC lilopelekwa sehemu ni kikosi kutoka South Africa,lakini kuna vikosi vya Malawi na Tanzania pia.
Msingi wa kisheria wa SADC kupeleka jeshi lake DRC uko katika mkataba wa makubaliano ya nchi wanachama ya mwaka 2003 yanayoainisha kwamba shambulio lolote kwa nchi mwanachama litatafsiriwa kama kitisho cha amani na usalama kwa nchi zote wanachama,na hivyo nchi zote zitashirikiana kuzima tishio hicho.
Kikosi cha SADC kilipewa jukumu la kuisaidia serikali ya DRC katika kurejesha amani na utulivu kwa kuisaidia kijeshi katika mapigano dhidi ya waasi na kunyang'anya silaha zao....,kwa maana nyingine siyo kikosi cha kulinda amani( peace keeping mission) kama vikosi vya UN ambavyo hukaa katikati ya mahasimu ili wasipigane.
Uzembe wa viongozi na watunga sera wa SADC ni kwamba,pamoja na kuvijua kwao kiundani vikosi vya waasi vilivyomo DRC,ikiwa ni pamoja na M23 na namna wanavyosaidiwa na Rwanda..na aina ya silaha walizonazo, ..lakini bado wakalifanya jeshi la SADC liingie DRC kama kulinda amani tu na siyo kimapigano.
Mathalan, walikubaliana kikosi cha wanajeshi 5000 kipelekwe kwa kuanzia,lakini wamepeleka askari 1300 tu wenye silaha za kulindia amani zaidi kuliko za mapigano kisasa katika uwanja wa vita.
Kichekesho ni kwamba wanajua idadi ya kikosi cha adui anazidi chao....,na wanajua pia aina ya silaha aliyonayo adui wanayekwenda kumkabili. Ni kama kuamua kwenda na mishale vitani,wakati unajua adui ana bunduki.
Kana kwamba haitoshi,kikosi cha SADC kinakosa hata kuwa na surveillance drones ...vifaa muhimu kwa jeshi la ardhini kwa sasa ambazo zingewawezesha kuona vikosi vya M23 vikifanya approach hapo mjini siku waliyoshambiliwa. Hata jeshi chovu la UN wanazo drones,japo kikosi chao hakipigani.
Ikumbukwe kuwa kikosi cha Umoja wa Africa(AU) ambacho kilihusisha pia Tanzania ,kilichokwenda DRC mwaka 2013 kwa lengo la kuwapiga waasi wa M23 kilijipanga kwa kazi hiyo...,na matokeo yake waasi wakapigwa na kukimbilia kwao Rwanda na Uganda.
Jeshi la SADC limepelekwa kama linaenda kupatanisha kati ya wagomvi wawili.
Watengeneza sera wa SADC waliweka siasa katika kutekeleza masuala ya kiufundi ya kijeshi kutokana na ubahili.
M 23 sio waasi bali ni Wanajeshi wazalendo wa kweli wanaopinga ubaguzi na utawala wa kishetani na wa kipumbavu wa Tshekedi .
Utawala unaoshindwa kutumia rasilimali nyingi zilizoumbwa na Mungu kwa ajili ya Waafrika wote usaidie binadamu wanaoishi ukanda wote wa eneo hilo bila ubaguzi.
Tshekedi kama ni mzalendo basi avue suti yake avae Gwanda za jeshi aende msituni apigane urais wake . Badala yake Mhuni na Fisadi Tsisheked anapanda ndege kwenda kula starehe Ufaransa kwa Wezi wenzake na kuwaacha Wanajeshi wake wasio na Maslahi wala mishahara ,wanajeshi wanaoishi kama manyani ndio wamsaidie kupigania maisha na starehe zake.
Pumbavu kabisa .
M23 ndio wazalendo maana wanapinga uhuni,ufisadi ,mauaji ya Raia ,na ubaguzi unaofanywa na Wezi wa rasilimali za Afrika .
Nchi za SADDC zilipaswa kuwasadia Raia wa Kongo kuondokana na ukoloni mambo leo unaofanywa na serikali kwa manufaa ya familia zao na wazungu wa Ufaransa na Marekani .
Wanataka Kagame na serikali yake Waingie kupambana na wazalendo na waafrika Wenzao badala ya kupambana na serikali ya Tsisheked ambayo ni hatari kwa nchi jirani ya Rwanda ,Watusi ,wahutu ,waganda ,waha na wahaya na amani ya Tanganyika .
Serikali iliyowekwa kifisadi ya Tsisheked ikiwafukuza Banyamulenge kutoka kwenye Ardhi yao basi amani ya Wananchi wa Rwanda ,Uganda ,Tanzania au Tanganyika itakua mashakani maana hao watu wote zaidi ya mil. 10 watakua hawana pa kuishi na kufanya shughuli zao halali za kufuga ,kuchimba madini ,kulima na uvuvi .
Ni marais vichaa tu ndio wanaoweza kupitisha azimio la kupambana na M23 . Marais wenye busara wataacha maamuzi ya ndani ya Kongo kufanywa na wakongoman wenyewe kushirikiana na wananchi.
Tsisheked nchi imemshinda . Rasilimali zote za Kongo unawezaje kuwafukuza waafrika wenzako tena wachapa kazi kama Banyamulenge . Ni bora angewafukuza Wanajeshi wake wote wanaume wote wakongomani wanaopaka hina kwenye vidole na kuva hereni huku wakitikisa makalio na kushindwa kulinda nchi yao dhidi ya Mabeberu wazungu wanaopora madini na kwenda kuinua maisha ya wazungu .
Wazungu ulaya wanategemea rasilimali kutoka Afrika ili wakuze uchumi wao na kuwalipa mpaka wale wasio na ajira lakini Afrika watawala wanawaza kujineemesha na familia zao peke yake .
Jeshi la Kongo linapaswa kuungana na M23 na kumtoa madarakani Tsisheked kwa lazima na kumrudisha Ufaransa aache Kongo ipate Watawala wa kijeshi na kuiendeleza Kongo.
Ni wakati sasa wa majeshi yote ya Afrika kuondokana na uhuni wa wanasiasa wanaoanzisha siasa za kipumbavu na kuwatumia wanajeshi na polisi kupigania ujinga na ufisadi uliofanywa na wanasiasa .
Jeshi la Kongo halina hadhi inayolingana na utajiri ulioko Kongo lakini wanasiasa wa Kongo ni mabilionea .
Wanajeshi wa Kongo amkeni mtetee rasilimali za Afrika na maslahi yenu yawe mazuri kama jeshi la Ufaransa na Marekani .
Rais na mawaziri wa Kongo wanaishi maisha ya anasa kuliko hata Trump halafu wanajeshi wake na polisi wanaishi kama mbwa na kuku wa kienyeji .Kuku wa kienyeji hapewi matunzo na mmiliki lakiniakitaga mayai mmiliki anakimbilia kuyachukua na hata vifaranga anavichukua na kujigamba kuwa ni vya kwake .
Marais wengi wa Nchi za kiafrika wameacha wafanyakazi na Wanajeshi na polisi wao kuwa na maisha ya kuku wa kienyeji huku wao (Watawala) wakiishi maisha ya peponi.
Kama watawala wa Kongo hawaoni adha ya yale yanayotokea Kongo basi hawawezi kamwe kuleta maendeleo wala kujenga nchi yenye Haki ,usawa na uzalendo kwa wote.
Hivi ni nchi gani yenye Rais mzalendo anayeshindwa kuunda jeshi lenye mafunzo ya kijeshi badala yake anagawa silaha kwa raia ili waue wananchi wenzao kwa misingi ya kikabila na kiitikadi . ?
Jeshi kazi yake ni kulinda mipaka ya nchi . Ni vipi silaha ziingiie Kongo na kuwafikia wananchi bila ya jeshi kujua ?
Marais wa nchi za SADDC wasijifiche kwenye mgongo wa M23 warudi kwenye nchi zao na warudishe majeshi yao nyumbani kwao kwa sababu tunajua kuwa UN na mabeberu wanaopora rasilimali za Kongo ndio wanaomwaga mapesa (dola ) kwa ajili ya kulinda wizi wao kwa kisingizio cha kulinda amani ya Kongo . Amani ya Kongo iko mikononi mwa wakongo na jeshi lao kumtoa Mtu mmoja na kakikundi kake kanakotumiwa na Mabepari wa ulaya Ufaransa na Asia kupora rasilimali za Kongo .
Kagame hahusiki zaidi ya kulinda nchi yake dhidi ya uvamizi wa Kongo unaofanywa kwa kisingizio cha Banyamulenge .
Hakuna Rais yeyote duniani anayeweza kukubali zoezi lolote la kuletewa Wafu zaidi ya mil. 10 kutoka nchi nyingine kwa kisingizio eti ni watu wa kabila moja na walioko kwenye nchi yake .
M23 ni wapigania Haki na watashinda na Kongo itakua huru na kurejesha amani yake kwa wakongo man wote bila kujali kabila,dini na rangi.