Uzi gani hutakaa uusome JamiiForums?

Uzi gani hutakaa uusome JamiiForums?

Page 94

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
5,204
Reaction score
15,207
Wasalaam Wakuu.

JF ni chuo kitaa. Unajifunza mengi mazuri na mabaya pia. Kama ambavyo chuo kuna kozi huwezi kuisoma, hata humu JF kuna nyuzi ambazo hutaki kuisoma kwa sababu moja ama nyingine.

Kichwa cha uzi kinabeba maana kubwa sana katika kumshawishi mtu kuusoma au kuupuzia. Na ndivyo ambavyo imekuwa kwangu.

Ukienda katika Jukwaa la JF Intelligence kuna uzi wenye kichwa 'Makosa 10 aliyofanya Mungu '

Pamoja na kuwa nauona kila siku sijawahi kuthubutu kuufungua. Binafsi, mimi ni muumi ni mkubwa sana kuwa Mungu yupo na ni muweza wa mambo yote kwa usahihi. Na hivyo, naamini Mungu hakosei katika maamuzi yake kwa utukufu alionao.

Ndiyo maana sikuona maana yeyote ya kuufatilia huo uzi. Pia, maandishi yana nguvu kubwa sana katika ushawishi. Kuusoma tu uzi ule kungeanza kujengeka picha katika ubongo wangu ni kwa namna gani Mungu alikosea na kufanya hivyo kungeanza kushusha kiwango cha imani yangu.

Hizo ndizo sababu zilizonifanya kuupuzia.

Je, wewe ni uzi upi ambao huwezi kuusoma na kwa sababu gani?
 
Back
Top Bottom