Uzi gani hutakaa uusome JamiiForums?

Uzi gani hutakaa uusome JamiiForums?

Mimi kuufungua uzi siyo ishu ila kuchangia.
 
Asalaam Alekyum!

Alhamdulillah, sijambo kabisa. Super mama naye yu buheri wa afya tele.

Mambo mengi, ila nipo. Kheri?
Jambo la kheri kaka.

Nafurahi kukuona tena.yep ni kheri.

Upo kule kule au ulishaondoka??
 
Sijawahi ogopa / kutotaka kufungua Uzi fulani, nafungua nasoma partially au siusomi kabisa ila nitapitia comments mbili tatu then naupotezea mazima.
Happy New Year.

Sasa mimi kusoma partially siwezi. Lazima niusome vema. Kama naona hauna maana naupotezea tu.
 
Jambo la kheri kaka.

Nafurahi kukuona tena.yep ni kheri.

Upo kule kule au ulishaondoka??
😂😂😂 Hata sijui tena kama nipo au sipo. Maana mara ya mwisho kuwasiliana sikumbuki nilikuwa wapi. Ko, huenda nipo ama nisiwepo.
 
Wasalaam Wakuu.

JF ni chuo kitaa. Unajifunza mengi mazuri na mabaya pia. Kama ambavyo chuo kuna kozi huwezi kuisoma, hata humu JF kuna nyuzi ambazo hutaki kuisoma kwa sababu moja ama nyingine.

Kichwa cha uzi kinabeba maana kubwa sana katika kumshawishi mtu kuusoma au kuupuzia. Na ndivyo ambavyo imekuwa kwangu.

Ukienda katika Jukwaa la JF Intelligence kuna uzi wenye kichwa 'Makosa 10 aliyofanya Mungu '

Pamoja na kuwa nauona kila siku sijawahi kuthubutu kuufungua. Binafsi, mimi ni muumi ni mkubwa sana kuwa Mungu yupo na ni muweza wa mambo yote kwa usahihi. Na hivyo, naamini Mungu hakosei katika maamuzi yake kwa utukufu alionao.

Ndiyo maana sikuona maana yeyote ya kuufatilia huo uzi. Pia, maandishi yana nguvu kubwa sana katika ushawishi. Kuusoma tu uzi ule kungeanza kujengeka picha katika ubongo wangu ni kwa namna gani Mungu alikosea na kufanya hivyo kungeanza kushusha kiwango cha imani yangu.

Hizo ndizo sababu zilizonifanya kuupuzia.

Je, wewe ni uzi upi ambao huwezi kuusoma na kwa sababu gani?
Kula tunda kimasihara
 
Kuna nyuzi sijawahi kuchangia ila naziona tu ,ule wa kula "kimasiara" na wa kupeana likes.
 
Happy New Year.

Sasa mimi kusoma partially siwezi. Lazima niusome vema. Kama naona hauna maana naupotezea tu.
Happy New year too jiranii

Me kusoma partially ndio zangu, hata huu wako nimesoma title, intro kidogo mpaka pale ulipo- bold nikaacha 😀😀
 
Huo uzi wa "makosa 10 aliyofanya Mungu" sijawahi kuuona, natamani content zake.
 
Happy New year too jiranii

Me kusoma partially ndio zangu, hata huu wako nimesoma title, intro kidogo mpaka pale ulipo- bold nikaacha 😀😀
Umekataa kuja kunisabahi jirani.
 
Hata wewe [emoji16]
Nimemfahamu Mungu wangu kwa namna ya kipekee kabisa... Nina imani thabiti juu yake na uwezo wake wa uumbaji.... Kumkejeli ama kum challenge kwangu ni kitu cha kuogofya mno...!!!
Hata kwenye ushirikina pamoja na kuwa tunaroga sana lakini lakini linapotajwa jina lake kuu tunasanda
 
Back
Top Bottom