Ingawa Wahenga waliwahi kusema kuwa Mteja ni Mfalme au Malkia!
Lakini Baadhi ya wateja maofisini na madukani huwa ni vichomi na vichefuchefu wakubwa!
Ukiachilia mbali baadhi ya watoa huduma kuwa chanzo cha kuchangia ukorofi wa wateja wao!
Zipo tabia mbali mbali za wateja wasumbufu kwa watoa huduma either kwa kujua ama kutokujua!
Tabia hizo za wateja husababisha watoa huduma kukereka, kukosa ari ya kazi au kufukuzwa/ kufunga kazi mapema!
Hapa nimekusogezea baadhi tu ya tabia za wateja zinazokera watoa huduma.

- Wateja wanafika ofisini au dukani wakiwa na majibu yao tayari; Wateja wa namna hii humpa tabu sana mtoa huduma kumuelewesha mteja hata wasifikie muafaka mzuri
- Wateja wanaojifanya Staff; Hawa ni sampuli ya wateja wanaojifanya ni wadau katika ofisi husika lakini hawajui A wala Z ya namna huduma wanayohitaji inavyotolewa kiasi cha kuzalisha usumbufu.
- Wateja wanaokuja kwa mikwara ya vyeo au kazi zao wanazofanya; Hii ni sampuli ya wateja wanaopenda huduma kwa migongo ya taasisi zao, Hufikia hata kuvaa gwanda zao ili imradi tu mtoa huduma aelewe wao ni kina nani, mbaya zaidi humlazimisha hata mtoa huduma asifuate taratibu halali ili wao wapate kwanza.
- Wateja wapelelezi; Hawa ni wale wateja wenye kutaka kujua kila kitu hata kama hawafaidiki nacho kwa wakati huo, Pasipo kujali foleni ya watu nyuma hutumia mda mwingi kwa mtoa huduma kuuliza kila kitu na ahadi lukuki, pia hupenda kurekodi rekodi watu kishamba.
- Wateja watongozaji; Hii sampuli nayo haivumi lakini imo, ni wateja wenye uwezo mkubwa sana wa kumzoea mtoa huduma kwa mda mfupi, hutumia mgongo wa customers care kupenyeza maombi yao ya ngono!
- Wateja wa ukabila na ukada! Hawa ni aina ya wateja ambao kila kitu wanataka kutumia ukabila au uchama ili kumlainisha mtoa huduma
- Wateja wapenda magumashi na njia za panya lakini hutaka risiti original; Dizaini hii ya wateja ni wale wanaopenda kupewa huduma kupitia mlango wa nyuma ili kurahisisha lakini hugeuka nongwa punde baada ya kuanza (Umbeya) kusimulia watu mbalimbali vile walivyopatiwa huduma kinyume na utaratibu kiasi cha kuhatarisha kazi za mtoa huduma.
- Wateja wendawazimu; Hawa ni wale wateja wanaofokea kila mtu hata kwa jambo dogo, wateja hawa hupenda kutoa mikwara na vitisho wakati mwingine kwa lugha chafu, ilihali wao hawapendi kujibiwa mbovu!