Uzi maalum kwa ajili ya tetesi mpya za One UI 9.5.

Uzi maalum kwa ajili ya tetesi mpya za One UI 9.5.

wisso1

Member
Joined
Jun 29, 2026
Posts
55
Reaction score
91
Habari za wakati huu wana JF, huu ni uzi mahususi kwa ajili ya kujuzana tetesi mpya za One UI 9.5 kwa kadri zinavyozidi kuvuja na kusambaa.

Ni takriban miezi mitatu sasa tangu Samsung walipoachia One UI 9.0 beta katika series za S26 katika baadhi ya maeneo.

Hata hivyo tukiwa tupo karibu kupata One UI 9.0 toleo thabiti (stable version) kwa watumiaji wote wa Samsung (eligible devices), zimeanza kuonekana tetesi mpya kuhusu One UI 9.5 ambayo itaachiwa rasmi mapema hapo mwakani pamoja na series za S27.
Screenshot_20260814_182218_X.png


Kutokana na tetesi zilizopo sasa One UI 9.5 italeta mabadiliko katika mwonekano wa UI nzima katika simu za Samsung.


Baadhi ya mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

1. Hatimaye Samsung wanaleta native app lock feature: kabla ya hapo haikuwezekana kabisa kuweka lock ya app moja moja.
Screenshot_20260814_182243_X.png
Mtumiaji alilazimika kutumia secure folder kwa ajili ya kuhifadhi baadhi ya vitu sensitive.
Ila rasmi sasa tutaweza kuset app lock katika kila application.

Screenshot_20260814_182245_X.png
2. Katika Screenshot zilizovuja zinaonesha ujio wa Glass-like design system wide; lakini hii ni tofauti na ile liquid glass ya apple, kwani Samsung wanabaki na design yao ya Frosted-glass.
Screenshot_20260814_182429_X.png
Design hii ya Samsung inaonekana kuwa na borders zenye kung'aa katika edge za floating bars.
Screenshot_20260814_182433_X.png
20260815_104954.jpg
Vilevile kitufe cha ku search katika phone app kimehamishiwa chini pamoja na controls nyingine badala ya kuwa juu, kama inavyoonekana hapo kwenye picha.
Screenshot_20260814_214753_X.png
3. Vilevile Icon ya battery na Network indicator zimeongezwa ukubwa ili kurahisisha kuangalia asilimia za battery na Network strength; Tofauti na ilivyokuwa kwenye One UI 8.5 ambapo icon ya battery ilikuwa ni ndogo kiasi, kama inavyoonekana tofauti hapo kwenye picha
Screenshot_20260815_114029_Gallery.png
4. Samsung rasmi wanaleta dark mode icons; Tofauti na ilivyo hivi sasa, Samsung hatimaye wameleta feature itakayobadilisha icons kuwa dark pindi utakapo set dark mode.
Screenshot_20260815_104744_Samsung Browser.png
Japokuwa hii hata kwenye One UI 8.5 ipo ila katika One UI 9.5 inaonekana Samsung wameamua kuwa serious kiasi.


Nitaendelea kuedit hii thread kwa kadri tetesi mpya za One UI 9.5 zinapokuwa zinasambaa

Amaut🤸‍♂️
 
Back
Top Bottom