Uzi maalum kwa shuhuda za miujiza

Uzi maalum kwa shuhuda za miujiza

Kalamu Yangu

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
1,107
Reaction score
1,056
Tumekuwa tukisikia na kuona miujiza mbalimbali ambayo imekuwa ikifanywa na viongozi wa dini na watu wengine wenye uwezo wa kufanya hivyo..
Zimevuma habari za watu fulani kuwaponya wagonjwa, kufufua wafu, kusaidia walemavu wa ulemavu tofauti kurejea katika hali ya kawaida...
Lakini kumekuwa na kundi kubwa la wakosoaji na wasioamini kuwa kama kuna kitu "miujiza" zaidi wakisema kuwa ni usanii tuu, wakihoji ni nani alimwona mlemavu ama mgonjwa anayemfahamu akifanyiwa miujiza zaidi ya kusikia na kuona kwenye vyombo vya habari?

Uzi huu utakusanya shuhuda za miujiza hiyo....ushuhuda wa kwanza ni wangu..

Nilishuhudia muujiza zaidi ya kumi iliyopita , mdogo wangu aliyekuwa akisumbuliwa na vidonda na maumivu kama ya moto ingawa hakuungua.Tatizo lilimsumbua kwa miezi zaidi ya mitatu akipata tiba mbalimbali hospitali bila kupona.
Wakati tukihangaika kupata ufumbuzi wa tatizo hilo, tukasikia kuwa ule msalaba (wa roman) unaozunguka dunia nzima ungepita kwenye kanisa lililokuwa jirani na tulipokuwa tukiishi.Ingawa hatukuwa wakatoliki ila siku ilipofika tukampeleka dogo akaushika ule msalaba kama wengine walivyokuwa wakifanya na kuanzia siku ile ile vila vidonda vikaanza kukauka na kupona kabisa...

Huu ni ushuhuda nilioushuhudia, niambie na wewe mwanaJF ni upi ushuhuda wa muujiza ulioshuhudia?....
 
Umesema mlitumia dawa mbalimbali, mojawapo itakua ilimsaidia akaanza kupona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muujiza mkubwa ni kuwa hai,wa pili ni miye kumtangaza Yesu humu,na kama haitoshi nakaribisha mialiko ya kuja kuhubiri katika yale makanisa yatakayoniita!
Cha msingi waseme wako wapi,na ninafikaje huko!
 
Miujiza nilioshuhudia ni risasi 38 kurushiwa kwenye gari ya TL na yupo hai ila mtekaji wa watoto kapigwa risasi moja na polisi kafa
 
Back
Top Bottom