Hongera Hongera Hongera ndo nachoweza kusema kwa hizi timu zilizofanikiwa kuiona 2018 tamu katika mioyo ya wapenda kabumbu [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
Ebhu tujikumbushe kwanza hawa wamisri na ufalme wao katika soka la Afrika miaka kibao ata kabla ya aliyewabeba leo hii huyu mwenye mguu wa gold hajazaliwa .....twende sawa ...... baada ya kufuzu fainali za kombe la dunia mwaka 1990 zilizochezwa kule nchini Italy. Na katika fainali Argentina akipigwa 1-0 dhidi ya West Germany(now days German).
Kundi F:
- England
- Egypt
- Republic of Ireland
- Netherland.
Baada ya kufuzu walisimamisha ligi yao ili kuipa nafasi timu ya taifa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa muda mrefu zaidi na kuongeza uelewano mkubwa. Mchezo wa kwanza 1990 kombe la dunia Egypt 1-1 Netherland, mchezo wa pili Republic of Ireland 0-0 Egypt na mchezo wa tatu England 1-0 Egypt. Na hapo aliambulia alama mbili tu katika kundi F.
Baada ya The Pharaoh kupata tiketi tu ya kucheza kombe la dunia nchini Italy mwaka 1990 chini ya Kocha mzawa Hayati Mahmoud El Gohary, ambapo mpaka sasa ni miaka 27 imepita na teyari Egypt wameshatumia makocha 19 (ikiwa 8 wakigeni na 11 Wazawa) baada ya El Gohary kuachia ngazi. Na hatimae kocha mgeni kutoka Argentina Hector Cuper amefanikiwa kuipeleka tena The Pharaoh katika kombe la dunia mwakani kule nchini urusi, baada ya makocha 11 Wazawa kushindwa alichokishinda yeye mwaka 2017.
Baada ya kupita kwa kizazi cha dhahabu cha Egypt. Kizazi cha kina Mohamed aboutreka, Mohamed Zidane, meteeb, Mohamed Barakat na wengine wengiii, ambao mafanikio na umwamba wao ulikuwa katika kulitawala au kutawala michuano ya kombe la nchi huru za Africa (Africa cup of National).
Kizazi kilichoonekana ni cha kawaida sana kwao ndicho kimekuja kuwarudisha kule walikowahi kufika miaka 27 ya mtu mzima iliyopita. Kama Mohamed Salah, Ramadan Sobi, Mohamed elnany pamoja na mkongwe El hadary wamekuwa ni pahala pa historia ya the Pharaoh mwaka 2017 baada ya kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Congo Brazzaville pale Alexandria... Lakini pia kizazi hichi kilifika fainali ya kombe la mataifa ya africa na kupoteza dhidi ya Cameroon mapema mwaka huu 2017.
Mwaka 2017 kundi E: kufuzu urusi 2018.
1- Egypt alama 12
2- Uganda alama 8
3- Ghana alama 6
4- Congo alama 1.
Katika michezo 5 aliyocheza Egypt kati ya michezo 6 ya kufuzu kumbe la dunia mwaka 2018. Kashinda michezo 4 na kupoteza mchezo 1 tu dhidi ya Uganda. Na mchezo wa mwisho ni dhidi ya Ghana kule Accra Ghana.
Magoli 2 ya Mohamed Salah ndio yamelipia tiketi ya Urusi na kuwafanya Misri wawe ni taifa la pili kufuzu kwa upande wa Africa baada ya Nigeria kufanya hivyo wikiend iliyopita.......
Hongera the Pharaoh.... Tuliwamisi na nyinyi mkajimisisha pia.....