nakumbuka kipindi niko chuo siku hiyo pale meeda sinza napata kilaji mida ya sa nne usiku kuna mdada mmoja mzuri pembeni ya meza yangu alikua ameketi peke ake nikamuomba ani join kwenye meza yangu,akaitikia wito bila hiyana tukaendelea kupata kinywaji kwa pamoja na stori mbili tatu. Haikupita hata nusu saa akaja njemba mmoja hivi hata sijui alikotokea akaniambia eti alikua akinitafuta siku nyingi kwanini natoka na demu wake..kabla hata sijamjibu nilikula kelebu moja matata kuja kukaa sawa nimebaki peke angu kwenye meza na simu(s6) niliyokuwa nimeishika mkononi sina,kilikua ni kitendo cha fasta sana kutoka nje hawaonekani kuna bodaboda akaniambia amewaona huyo jamaa na mwanamke wameondoka na bodaboda pale mda sio mrefu nikabaki nimeduwaa tu pale. Baadae nilimueleza meneja wa bar akaniambia huyo jamaa anaitwa 'van dame' ndo huwa anatumia staili hiyo kuibia watu na wengi wameshalizwa