Uzi maalum kwa tuliowahi kuibiwa simu.

Uzi maalum kwa tuliowahi kuibiwa simu.

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Wakuu naomba tupeana uzoefu hapa kwa sie tuliowahi kuibiwa simu,,
Ilikuaje ukaibiwa , ulijisikiaje na ulireact vipi hii itapelekea kujifunza namna ya kuepuka kuibiwa tena na namna ya kufanya baada tu ya kugundua ushaibiwa.
Binafsi mwishon mwa mwezi June mwaka huu niliibiwa sim LG G5 , niliacha chaji sehem isiyo salama ikabebwa. Nilichanganyikiwa na mpaka Leo bado nina maumivu.
 
Wezi wanabadisha mbinu za kuiba kulingana na mazingira hakuna uzoefu ndg yangu mimi waliniibia mchana jua linawaka. Walichofanya ni jambo rahisi tu,nilitoka sokoni mikono yote miwili nimebeba mzigo nikawa natembea simu iko kwenye mfuko wa shati,wezi walikuwa watatu, wakagawana wawili wakaenda uelekeo niliokuwa naenda moja akanifuata kwa nyuma,wale walioenda mbele wakarudi tukakutana mahali njia ni nyembamba yule wa nyuma akanikanyaga kwa nyuma ile nageuza shingo kuangalia kuna nini,wale tuliokuwa tunapishana moja kulia kwangu moja kushoto wakanichomoa simu wakati yule aliyekanyaga kwa nyuma ananiomba msamaha kwamba amenikanyaga bahati mbaya kwa vile alikuwa na haraka huku aiwa anaendelea kwenda kwa mwendo wa haraka na wale tuliopishana nao pia wakaenda na haraka zao mimi muda wote sikujua picha inayochezwa,nilipobaki peke yangu nikawa nafikiria kilichofanyika siyo kitu cha kawaida ndiyo naangalia mfukoni simu hakuna, nikataka kuwakimbilia wale niliopishana nao siwaoni,nataka kumkimbiza aliyenikanyaga kwanyuma akanipita naye kashapotea nika baki naombolezea simu yangu ya laki 5 we acha tu usinikumbushe tena.
 
Hata Mimi.mpigo huu ulinitokea pale Kariakoo. Haikuniuma sana maana ile simu nilishaitumia zaidi ya miezi 7. Ilinichukua muda mpaka kununua smart nyingine. Wanacheza na body posture hatar
 
Mie kwanza niliibiwa huawei morogoro pale Rock garden yani niliibiwa ndani kabisa nilianzisha varangati hawatakaa nisahau, mtu unalipa kiingilio afu mwizi anakupora simu ndani.

Ya pili techno dah niliibiwa katikati ya kimara mwisho na stop over hapa niliibiwa kwenye gari ile nimesema nishushe kioo niachane na ac na kulikuwa na foleni basi mwizi nae akaniwahi. Ila kama kwenye gari kungekuwa na mwanaume tungempata ila ndiyo hvyo tulikuwa wanawake watupu tukaishia kupiga kelele basi.
 
Rock Garden pazuri.
 
kumbe sometimes huwa mnakiri kuwa nyie ni wadhaifu.... mnadai haki sawa kwa nn
 
Nlikuaga naonaga watu wanaosema wameibiwa cm ni wazembe sn mpk pale nlipoporwa na watu waliokua kwny boda boda
 
Majanga ya simu kama kuna mtu hajawahi kuibiwa sijui... Sipendi hata kukumbuka kioo kidogo cha gari kubomolewa na Beg dogo kuibiwa gari ikiwa parking na ndani kuna laptop, simu, passport,tiket,card zote.... We acha tu. Mungu tu ndiye anajua kilichoendelea.
 
nakumbuka kipindi niko chuo siku hiyo pale meeda sinza napata kilaji mida ya sa nne usiku kuna mdada mmoja mzuri pembeni ya meza yangu alikua ameketi peke ake nikamuomba ani join kwenye meza yangu,akaitikia wito bila hiyana tukaendelea kupata kinywaji kwa pamoja na stori mbili tatu. Haikupita hata nusu saa akaja njemba mmoja hivi hata sijui alikotokea akaniambia eti alikua akinitafuta siku nyingi kwanini natoka na demu wake..kabla hata sijamjibu nilikula kelebu moja matata kuja kukaa sawa nimebaki peke angu kwenye meza na simu(s6) niliyokuwa nimeishika mkononi sina,kilikua ni kitendo cha fasta sana kutoka nje hawaonekani kuna bodaboda akaniambia amewaona huyo jamaa na mwanamke wameondoka na bodaboda pale mda sio mrefu nikabaki nimeduwaa tu pale. Baadae nilimueleza meneja wa bar akaniambia huyo jamaa anaitwa 'van dame' ndo huwa anatumia staili hiyo kuibia watu na wengi wameshalizwa
 
nakumbuka kipindi niko chuo siku hiyo pale meeda sinza napata kilaji mida ya sa nne usiku kuna mdada mmoja mzuri pembeni ya meza yangu alikua ameketi peke ake nikamuomba ani join kwenye meza yangu,akaitikia wito bila hiyana tukaendelea kupata kinywaji kwa pamoja na stori mbili tatu. Haikupita hata nusu saa akaja njemba mmoja hivi hata sijui alikotokea akaniambia eti alikua akinitafuta siku nyingi kwanini natoka na demu wake..kabla hata sijamjibu nilikula kelebu moja matata kuja kukaa sawa nimebaki nimebaki peke angu kwenye meza na simu(s6) niliyokuwa nimeishika mkononi sina,kilikua ni kitendo cha fasta sana kutoka nje hawaonekani kuna bodaboda akaniambia amewaona huyo jamaa na mwanamke wameondoka na bodaboda pale mda sio mrefu nikabaki nimeduwaa tu pale. Baadae nilimueleza meneja wa bar akaniambia huyo jamaa anaitwa 'van dame' ndo huwa anatumia staili hiyo kuibia watu na wengi wameshalizwa
nimecheka kaa mazuri pole sana mkuu
 
Chali angu aliibiwa simu humu humu jf na raia inaitwa deimosi ata picha yake nliituma jamaa ni mngese sana mamaye , na pia msela wangu aliibiwa simu beach mida ya jioni aise beach sio kuzuri haswa mida ya jioni au mchana ukiwa umekaa kindezi ndezi
 
Simu yangu ya mkopo ili ibiwa kwenye basis LA Kilimanjaro express
Kitendo cha kuiweka juuu ya mapaja nikiwa naskiza mziki wakati was safari nikapitiwa na usingz kuja kushtuka nine baki na head phne
 
Back
Top Bottom