jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,530
- 9,550
Habari wana jamvi, uzi huu ni maalum kwa wale wanzangu ambao walipitia wakati mgumu kwa jambo moja au lingine kisha kuona mwanga ili iwe kama chachu kwa wenzetu ambao wamekata tamaa ya maisha hali ya kuwa wanauhai
KISA CHANGU
Kwa umri wangu syo mkubwa kabisa ,lakini ni kijana ambae nilikuwa na bado nina ndoto za kufanya mengi katika maisha hasa kusaidia watu.Safari yangu ya kutafuta maisha kwa nguvu zote ilianzia mwaka 2015,baada ya kuhitimu elimu yangu ya astashahada ya utawala.
Baada ya kukaa muda mrefu bila ajira nikaamua kwenda kumtembelea ndugu yangu mkoani kigoma kwa njia ya mabasi ya Saratoga.
Saa 11 asubuhi gari iliondoka pale ubungo naweza kusema kuwa huo ndo ulikuwa mwanzo wa misukosuko, hasa pale tulipofika Tabora tulikuta pori kubwa sana lakini mwanzo kabisa tukakutana na askari wengi sana wakiwa na magari yao, akaingia mmoja na kutuambia kuwa mbele kuna uwezekano mkubwa sana wakuwepo na waasi kwani jana yake walikuwa wanafyatuliana risasi na polisi.
Basi wakaingia askari wawili wakiwa na silaha nzito na magazine za kutosha,ndo mara yangu ya kwanza kuona askari wakibongo wakiwa wanatisha kiasi kile.
Basi wale askari wakatuambia kuwa gari itaondoka kwa kasi kidogo hvyo tufunge mikanda na wenye kuomba sala zao tuombe kabisa,dah nakumbuka siku hyo niliomba mpka maskio yalikuwa yanaongea[emoji28][emoji28][emoji28].
Safari ikaanza huku wale jamaa wakizikoki bunduki mle mle ndani kisha wakalala kwenye ile njia ya katkat ya ndani ya basi huku wakimuamuru dereva aendeshe spidi mpka mwisho,pasipo kusimama kwa jambo lolote.
Dah naweza kusema yule dereva alikuwa vizuri mno kwani gari ilikuwa iliendeshwa moka spidi ya mwisho huku ikitoa alarm ya hatari gari zima tukiwa kimya huku sauti zilizokuwa zinaskika ni yesu na muhammad tu,maana kwa ile spidi ile gari ingegonga hata tufali tu basi ingekuwa mwisho wa maisha yetu.
Gari ilitembea kwa spidi hyo mpka tunamaliza misitu mirefu kama hiyo zaidi ya mi nne,hatimae tukatoka salama,ashukuriwe mungu.Mungu si athumani tukaingia kigoma salama mida ya saa 5 asubuhi.
Lengo la kwenda Mkoa wa kigoma ni kwenda kujifunza tiba mbadala kutoka kwa babu wa rafiki yangu,Nilipokelewa vizuri sana na kwa ukarimu mkubwa sana kutoka kwa watu wale wa kigoma.
Nilijifunza vingi sana kuhusu tiba za asili baada ya miezi 6,alikuja mtu kutoka Congo na kuvutiwa na jinsi nilivyokuwa muelewa kwa haraka katika tiba asili hivyo akanichukua na kunipeleka kwao congo,ili nikajifunze mengi kuhusu tiba asili.
Huko ndiko kulikofanya maisha yangu yabadilike kwa mambo ya ajabu na mateso ambayo leo hii ningekuwa marehemu hakika sitaisahau misitu ya goma,
nitarudi...