Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Mwambie huyo Mungu wako unayedai yupo aje hapa mwenyewe ajidhihirishe yupo.

Kwa nini una hangaika kumtetea na kumwelezea?
Mungu ni nomino ya dhahania kama njaa, wewe unaweza kuiita njaa ikaja

Je kwakuwa haiwezi kuja haipo?
 
Sasa elimu ya mazingira ni ya wazungu tu?

Theology ni elimu kuhusu Mungu na Dini.

Ambapo hata mababu zetu wa kiafrika walikuwa na Theology zao kuhusu dini zao na Miungu yao.

Hivyo kusema Sayansi na Theology ni vya mzungu ni UONGO.
Hizo fact unazozielezea kisayansi hiyo elimu umeitoa wapi means umeisoma wapi? Na nani alikujuza kuhusu neno science? Je mababu zako wa millenia huko usukumani wanalielewa hilo neno science automatically au hadi ukawafundishe?

Je wewe huo ufahamu wa neno science umeutoa wapi?
 
Mungu ni nomino ya dhahania kama njaa, wewe unaweza kuiita njaa ikaja

Je kwakuwa haiwezi kuja haipo?
Njaa haiwezi kuja kwa vile haipo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika tu.

Hata huyo Mungu hayupo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika tu.
 
Sasa elimu ya mazingira ni ya wazungu tu?

Theology ni elimu kuhusu Mungu na Dini.

Ambapo hata mababu zetu wa kiafrika walikuwa na Theology zao kuhusu dini zao na Miungu yao.

Hivyo kusema Sayansi na Theology ni vya mzungu ni UONGO.
Mimi babu yangu hakuamini Mungu bana babu yangu aliamini Mizimu na matambiko ambayo siyo Mungu

Mungu tumekuja kufundishwa na wavamizi na ndio maana zile mila za kutambika dini inakataza
 
Unaingia jamii forums, mada za dini
Mdini: mungu yupo
Atheist: why?
Mdini: coz sijui jua limetoka wapi

Kwa akili hizi mwacheni mwamposa ajaze viwanja vya kawe na acheni china waende mwezini..bongo bado sana
Wataka kuniambia ulaya hawaamini uwepo wa Mungu?
 
Njaa haiwezi kuja kwa vile haipo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika tu.

Hata huyo Mungu hayupo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika tu.
Kama ndio hivyo science pia ni elimu ya uwongo maana inadanganya kuwa kuna upepo wakati upepo haupo ni neno la kufikirika tu
 
Sasa huo ukweli utaujuaje 🤔 uku unaambiwa umkiri mtume Muhammad na uku umkiri yesu kristo ndio njia ya mbinguni 🤔
 
Mimi babu yangu hakuamini Mungu bana babu yangu aliamini Mizimu na matambiko ambayo siyo Mungu

Mungu tumekuja kufundishwa na wavamizi na ndio maana zile mila za kutambika dini inakataza
Soma historia vizuri waafrica walikuwa na miungu yao waliokuwa wanaiabudu, mfano olodumare, chukwu, ngai, Warumbe, Mukasa, Sangoma n.k
 
Kuna mwenzio anasema science haihitaji kuaminiwa naona wewe umesema waiamini waeza kutolea ufafanuzi kwanini unaiamini?
 
Mimi babu yangu hakuamini Mungu bana babu yangu aliamini Mizimu na matambiko ambayo siyo Mungu
Unathibitishaje Mizimu sio Mungu?

Na unathibitishaje Mungu sio Mzimu?

Kwa nini unasema babu zako wali amini mizimu?

Kwa nini husemi wazungu wali amini mizimu pia?
Mungu tumekuja kufundishwa na wavamizi na ndio maana zile mila za kutambika dini inakataza
 
Infropreneur​

Tuvutana huku, kule.. swali ni Moja tu, yupo anaeweza kuthibitisha uwepo wa Mungu?
 
Kwa sababu inaweza kuthibitika, ndio maana naiamini
Mfundishe uyu

Infropreneur​

Ajue kuwa science pia ni imani kama ilivyo theology utofauti unakuja kwenye how to verify them
 
Mfundishe uyu

Infropreneur​

Ajue kuwa science pia ni imani kama ilivyo theology utofauti unakuja kwenye how to verify them
Science sio Imani, ni kitu halisia, na ndio maana dini na sayansi ni vitu visivyochangamana, sababu dini ni nadharia tu...
 
Mfundishe uyu

Infropreneur​

Ajue kuwa science pia ni imani kama ilivyo theology utofauti unakuja kwenye how to verify them
Aliyekwambia sayansi ni imani ni nani?

Hebu leta andiko lolote linalosema sayansi ni imani.
 
Mkuu wewe unaiamini science kama wengine wanavyomuamini Mungu

Wewe una uhakika gani kuna gravitational force ushawahi kuishika au kuihisi? Au unaiamini tu kuwa ipo kwakuwa umesoma vitabu vya uongo vya science vinavyotumia shuhuda za kiungu kuthibitisha?
 
Mfundishe uyu

Infropreneur​

Ajue kuwa science pia ni imani kama ilivyo theology utofauti unakuja kwenye how to verify them
Na mara nyingi dini huwa inaipinga sayansi, kwa maana sayansi imekuja kujibu maswali yaliyokuwa yanajibiwa na dini tu enzi izo mfano, watu walikuwa wanaomba mvua inyeshe, siku iz tunajua mvua itanyesha tu kwa msimu, na hailetwi na Mungu, au zamani kabla ya sayansi ya tiba kugundulika, wagonjwa walikuwa wanaenda kwa wahubiri, ila sayansi siku iz imetuletea hospitali na dawa Bora. Ko sayansi imetokea kui challenge dini na ndio maana mtu wa dini huwa sio rahisi kuamin sayansi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…