Dah! Mtu mzima nimekwama wallahi!
Kuna mwanamke nampenda sana yaani ni ile mno kabisa kabisa wani handredi pasenti. Nimefanya kila njia ili niweze kumtoa moyoni imeshindikana. Nimejaribu hata njia za kunifanya pengine nimchukie (au yeye anichukie) lakini wapi. Nikisikia tu sauti yake mie huyoo hoi dah!
Na huu ni mwaka karibia wa tatu nahangaika. Na wanawake wengine yaani nawaona kama takataka tu hata kama wana vigezo vyote nivitafutavyo; na kuzidi.
Huwa wanasema time is the best doctor ila kwa hili nahisi kama time is doing the opposite...the more time elapses, the more I fall for her deeper and deeper.
Kuna mtu aliyewahi kukutana na hali hii? Yaani unampenda mtu mpaka unakwama kujichomoa? Suluhisho lake ni nini?
Mwanamke mwenyewe anatokea Tanga. Au kaniroga huyu maana kha!🤪
View attachment 3181228