Uzi maalum kwa wapenzi wa Muziki mzuri

Uzi maalum kwa wapenzi wa Muziki mzuri

Kutoka kwenye album yake Ngiama Noel a.k.a wereason iitwayo Kibuisa mpimpa au Operation dragon ya mwaka 2001.
iu

album hii yenye nyimbo takribani 16, inabeba nyimbo kali za rhumba kama 13 ans(miaka 13), blandine, le grande mansiuer, annie, wakawaka na moja niipendayo zaidi iitwayo UN PRINCE AU CONGO ('MFALME' WA CONGO). Nyimbo hii wera alimuimbia rafiki yake tajiri aliyeitwa ALICI BABA. Jamaa alikuwa tajiri mwenye kupenda maisha ya kifahari sana. na pia mpenzi mkubwa wa muziki wa kikongo na hasa werason.
ALISI-BABA.jpg

Huyo ndie alici baba. kwa sasa ni marehemu na alifariki mwaka 2013.

kwenye video hii utamuona Baby Ndombe-ambaye ni mmoja wa vocalist wa WMMM wa enzi hizo kabla hajamkibia wera mwaka 2004 katika kipindi ambacho wera alikimbiwa na karibu 90% ya waimbaji-akiigiza maisha ya alici baba burudika na nyimbo hii.
 
Back
Top Bottom