Uzi Maalum wa kipi ulidanganya utotoni

Uzi Maalum wa kipi ulidanganya utotoni

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Nikiwa Mdogo mama yangu aliniambia watoto hununuliwa hospitalini

Bibi yangu aliniambia eti nikimchungulia mti akiwa uchi nitajikuta juu ya mti mkubwa na sitaweza kushuka hii iliniogopesha ila Leo najua sababu


Karibu na nyumbani kulikuwa na msitu mnene hivi kama kilometa mbili hapo baba aliniambia eti katika maitu ule kuna nyoka mwenye vichwa saba.

Kuna wadudu flani hivi tuliambiwa kuwa ukiwachezea eti wanailukia puani na huwezi kuwatoa


Ni mengi sana ya wanyonya damu na mikwala kibao leo tumekua tunagudua yalikuwa ni makatazo ya kutuonya kisaikolojia.


Wewe ulidanganywa nini utotoni

Karibu
 
Back
Top Bottom