"Kwa wale askari wetu jasiri, nawaongelea nyinyi polisi, baraka za mola wetu ziwamulike, muwalinde watanzania na Mali zao dhidi ya adui wa ndani, nyinyi ni moja kati ya nguzo za nchi, taifa linawatumainia, hata wale wanaofanya kejeli dhidi yenu wanafanya hivyo kwakuwa nyinyi mpo. Kukosekana kwenu, kuzembea kwenu, uonevu wenu, ulaji rushwa wenu utakwaza taifa lenu. Kila la kheri kwenye jukumu lenu"