Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

nimekopi mahali:
CHEKA KIDOGO NA MATENDO YA WANADAMU WA SIKU ZA MWISHO
Baba mmoja alikuwa na mfanyakazi wake wa ndani aitwaye Bakari (house boy); mara nyingi Bakari huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue

Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika Sikumoja bosi huyu aliamua kununua wine fulani ambayo ukiongeza maji inabadirika rangi Kama kawaida, Bakari akanywa ile wine na akaongezea maji, baada ya muda ikabadirika rangi; bosi akaja kugundua Bakari alipostukia hali ya hewa, akaenda jikoni kujibana

Mara mzee akaanza kumwita, fuatilia

Boss: Bakariiii!
Bakari: Naam baba!
Boss: Nani kanywa wine yangu?
Bakari: Kimyaaaa (hajibu kitu!) Boss: Bakariiiii !
Bakari: Naam baba!
Boss: Nauliza, nani kanywa wine yangu halafu anajazia majiii?
Bakari: Kimyaaaaa! (Hakujibu kitu)

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni

Boss: Kwanini nikikuita jina unaitikia, ila nikikuuliza kuhusu wine yangu unanyamaza?
Bakari: Baba, huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa; lakini maneno mengine husikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni harafu nijaribu kukuita

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita

Bakari: Babaa!
Boss: Naam Bakari!
Bakari: Mida ya saa sita za usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss: Kimyaaaa! (hakujibu kitu)
Bakari: Baba babaa!
Boss: Ndio Bakari!
Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss: Kimyaaaaaaa! (hakujibu kitu)

Boss akatoka nje: Aisee, Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina, duh

Mama akasema msinizingue nyie Mbona siwaelew

Bakari: Mama kama huamini na wewe ebu nenda uone

Mama akaenda jikoni

Bakari: (akaita) Mamaaaa
Mama: Bee Bakari
Bakari: Eti hiyo mimba uliyonayo ni ya baba au yangu?
Mama: Kimya
Bakari: Mama nakauliza tena, hiyo mimba ni ya baba au yangu?

Mama huku anatoka nje: Aisee!!! kweli hili jiko inabidi lichunguzwe vizuri, humu unasikia jina tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…