Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka usafini WCB, Harmonize amesema kuwa wakati anaandika wimbo 'Sina' nafasi ya main character alitaka acheze Dallas ambae ni EX boyfriend wa @wolperstylish . . Harmonize alisema hayo kupitia clouds fm ambapo alidai wakati anaandika wimbo huo alikuwa pamoja na @Youngkillermsodokii ambae ndiye aliyependekeza Mr Nice kuwepo katika Video ya wimbo huo. . . "Wakati naandika wimbo nilikuwa pamoja na Young killer wimbo ulikuwa unataka mtu aliyekuwa na pesa zamani lakini kwa sasa amefua. Mimi nilitaka kwenye video awepo Dallas lakini Young killer akaniambia Dallas wabongo wengi hawamjui kwa sura wanamjua jina tu, young killer hata hajafikiria sana akanitajia Mr Nice mwenyewe nilishtuka kwanza" alisema harmonize . . Aidha muimbaji huyo wa bongo fleva ambaye kwasasa anatamba na kibao chake kipya 'Sina' ameongeza na kusema kuwa kuna project zingine Mr nice kafanya na wasanii wengine wa WCB. .
 
Mtangazaji wa kipindi cha familia Faiza Ally amesema yupo tayari kupiga picha za utupu endapo mtu anayemtaka kupiga picha hizo atafikia dau analolitaka kama Mil 100 Aliyaongea hayo alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Shilawadu Clouds FM kuwa atapewa milioni 6 ili apige picha hizo...lakini akadai kwa million 100 yupo tayari
 
WAKATI mashabiki wakiwa bado wanamshangaa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Massawe‘Wolper’ juu ya tabia yake ya kubadili wanaume kila kukicha, katika hali ya kushangaza, ameibuka na kudai kuwa ataendelea kubadili wapenzi, muda wowote atakapogundua kuwa aliyenaye, hana vigezo. Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wolper alisema hawezi kuogopa maneno ya watu wanayosema juu yake kwa vile hawaelewi anachokumbana nacho katika mapenzi, kwani hawezi kung’ang’ania kukaa kwenye uhusiano ambao haendani nao au unampa shida. “Unajua unapokuwa na mpenzi huwezi kujua kuna tabia utakumbana nazo ambazo haziendani na wewe, lakini pindi unapogundua ni bora kuondoka kuliko kukaa sehemu ambayo huna furaha nayo,” alisema Wolper. Staa huyo aliongeza kuwa hata mtu aliyenaye hivi sasa endapo atagundua kama tabia hazirandani, ataangalia ustaarabu mwingine kwani haogopi kusemwa kuhusu kubadilisha wapenzi.
 
[HASHTAG]#HABARI[/HASHTAG] - Jennifer Kanumba adaiwa Kuwa too busy na mitandao badala ya kula kitabu zaidi !! . Star huyo wa Filamu za Uncle JJ, This Is It na Zena na Betina anaingia kidato cha 6 mwaka huu baada ya kufaulu kidato cha 4 hivyo kuendelea na form five. . . Toa ushauri wako kwa Jennifer kanumba
 
NDOA YA SHILOLE KUFUNGWA HIVI KARIBUNI- "Ni kweli nimechumbiwa na Mwenyezi Mungu akijaalia nitafunga ndoa. Mama yangu Khadija Kopa ndio atakuwa somo wangu." - BY @shilolekiuno_badgirlshishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…