Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwaka 2008, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa,(FAO) lilitangaza kuwa, ulimaji wa muhogo waweza kuepusha mabaa ya njaa na kuwa chanzo cha nishati katika nchi zenye matatizo ya chakula na kukabiliana na bei ya mafuta ya nishati.
 
Hata hivyo zao hili liliendelea kudharauliwa na kuonekana ni mzizi wa hamu na chakula kwa maskini.
Baada ya muda mfupi, Afrika imeshuhudia, watu zaidi ya 11 milioni wakikumbwa na janga la njaa katika pembe ya Afrika (Somalia, Sudan, Kenya) mwaka huu ilhali suluhisho lilikuwepo mikononi mwetu.
 
Wakulima wakubwa kwa wadogo hapa Tanzania, bado hawajatambua manufaa ya kiuchumi ya muhogo. Hali kadhalika viwanda vyetu vya uzalishaji navyo havina habari za manufaa yake.Eustice Kasembe, mkulima, kijijini Chikunja Wilayani Masasi anasema, zao la muhogo hutumika zaidi kwa ‘matamba’(ugali) kijijini hapo na si vinginevyo.
 
Hatuuzi kabisa zao hili, hata kwa wanaokula ‘matamba’ ni pale wanapokosa unga wa mahindi,” anasema Mzee Kasembe. Katika wiki ya kilimo cha muhogo iliyoendeshwa hivi karibuni hapa nchini wadau wa kilimo wanasisitiza ulimaji wa muhogo.
 
Wanahamasisha kulima zao hilo linaloweza kustawi katika ardhi isiyo na rutuba, kuvumilia ukame na lisiloathiriwa kwa urahisi na magonjwa ya mimea kama ilivyo kwa mazao mengine. Waziri wa Kilimo na Chakula, Jumanne Maghembe, analitaja zao hili kuwa ni la pili katika kuchangia uchumi wa taifa kwa asilimia 19 baada ya mahindi.
 
Faida hizi humtoa mkulima katika wasiwasi wa kutumia fedha za kununulia dawa za mimea.
Meneja wa Taasisi ya Kuongeza Thamani ya Muhogo Afrika, Grace Mahenga, anatoa takwimu na kusema: Tanzania inaweza kuokoa dola za Marekani 20 milioni sawa na Sh32 bilioni zinazotumika kuagiza chakula nje, endapo itaendeleza zao la muhogo.
 
Zao hili likipewa kipaumbele, linaweza kuongea kipato cha mkulima mmoja mmoja, wafanyabiashara, na ni faida kwa taifa zima” anasema Mahenga.Muhogo ni zao lenye faida nyingi kijamii na kibiashara. Ni zao ambalo ni malighafi ya kuzalisha zaidi ya bidhaa 300 zikiwemo za chakula na zile ambazo siyo za chakula viwandani.
 
Katika viwanda, mazao yanayopatikana katika mzizi wenyewe, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai. Baadhi ni vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki.Vilevile wanga wa muhogo hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup).
 
Katika viwanda, mazao yanayopatikana katika mzizi wenyewe, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai. Baadhi ni vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki.Vilevile wanga wa muhogo hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup).
 
Katika viwanda, mazao yanayopatikana katika mzizi wenyewe, miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai. Baadhi ni vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na plastiki.Vilevile wanga wa muhogo hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari (sugar syrup).
 
Anasema kwa kujiamini kabisa kuwa “ninazalisha karibu tani 330 za muhogo. Tunauza unga kiasi cha Sh100 kwa kilo sawa na Sh1,700 za tanzania,” anasema Masyuki na kuongeza kuwa: “hata hivyo mahitaji kwa sasa ni mengi kuliko uzalishaji.”
 
Takwimu za kilimo cha muhogo duniani zinaonyesha kuwa, Afrika ni bara la tatu duniani kwa kuzalisha zaidi muhogo. Karibu tani milioni 102.6 huzalishwa barani humu kila mwaka.Kwa uzalishaji huu, Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika, hazina budi kupiga kengele zaidi ili kuliimarisha zao hili kibiashara kama nchi nyingine zifanyavyo.
 
Kwa mfano, Thailand, ambayo haizalishi muhogo kwa kiasi kikubwa kama Tanzania, imelipa kipaumbele zao hilo na sasa limekuwa ni zao kuu linaloleta fedha za kigeni nchini humo.

Thailand, huuza unga wa muhogo katika nchi za Ulaya kwa ajili ya chakula cha wanyama na nishati ya mafuta (biofuel). Leo hii, nchi hiyo ndiyo inayoongoza duniani kwa kuuza mazao yake ya kilimo nchi za nje.
 
Kwa wingi wa bidhaa zinazoweza kuzalishwa na zao hili na kwa sifa za uvumilivu wake wa ukame na maradhi, watanzania hawana budi kulipa kipaumbele. Wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda wanatakiwa wachangamkie fursa zinazopatikana katika mzizi na majani ya mti huu.
 
Juhudi mbalimbali za kukuza kilimo cha muhogo zinazoendelea kitaifa na kimataifa zinawalenga wakulima, wafanyabiashara na wenye viwanda (wazalishaji). Muungano wa Mapinduzi ya Kijani Afrika(AGRA) pamoja na Shirika la Kilimo la Kimataifa (FCI), limeanzisha mradi wa kukuza kilimo cha muhogo Afrika Mashariki. Muungano huo umelenga vijiji zaidi ya 30,000.
 
Hata hivyo wadau wa kilimo wanatakiwa kuhakikisha yanakuwepo mazingira bora kwa mkulima ili aweze kuzalisha kiasi kikubwa cha zao za muhogo. Ili sifa za shujaa huyu zionekane, wakulima hawana budi kuwekewa mazingira safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…