Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

faida mbalimbali za kutumia aina tofauti za chai kiafya.

Tunaposema aina tofauti za chai ni kwa sababu pamoja na maeneo mengi nchini kutumia majani ya chai aina ya rangi nyeusi, kuna aina mbalimbali za rangi ya majani, ambayo kwa mujibu wa wanasayansi yana faida tofauti tofauti za kiafya.

CAMOMILE TEA

Wanasayansi wamegundua kuwa chai aina ya Camomile inawasaidia wanawake kuishi maisha marefu.
 
Aidha si hilo tu, bali inasaidia kudhibiti kiharusi, lakini pia ni tiba ya ngozi kutokana na kuwa na sifa ama tabia za kumng’arisha, ikiwa ni pamoja na kulainisha ngozi ya mtumiaji.

CHAI YA JANI LA KAHAWA (COFFEE LEAF TEA)

Mwaka 2013, Wanasayansi waligundua kwamba chai iliyotengenezwa kutokana na majani ya mimea ya kahawa ina kiwango kikubwa cha misombo iliyo na manufaa makubwa kwa afya ya binadamu.
 
Mmoja wa Wanasayansi hao, Dk. Aaron Davies anasema kwamba: “ Kilichoshangaza zaidi ni kwamba, chai itokanayo na mimea ya kahawa ina kiwango kikubwa cha antioxidants kuliko ilivyo kwenye chai iliyotengenezwa na majani ya chai ya kijani au chai ya kawaida itokanayo na majani yenye rangi nyeusi.

Aidha majani ya chai yatokanayo na mimea ya kahawa ndiyo hasa yaliyo na kiwango kikubwa ya kemikali aina ya 'mangiferin' ambayo inajulikana kwa manufaa yake mengi ya kiafya kwa binadamu.

Kemikali hii imegundulika kupunguza kwa kiwango kikubwa hatari za kuugua ugonjwa wa kisukari na chelestrol kwenye damu, wakati huohuo ukiulinda ubongo.
 
CHAI YA KIJANI (GREEN TEA)

Wanasayansi wanasema, chai ya kijani ina kiwango kikubwa cha kiini kiitwacho polyphone ambacho kina manufaa kwa afya ya binadamu.

Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha antioxidants ndani ya majani ya chai ya kijani, kunasaidia kudhibiti athari za magonjwa ya saratani za matiti, mapafu na tumbo.

Aidha inadaiwa kwamba kikombe kimoja cha chai ya majani ya kijani inaweza ikamlinda mnywaji dhidi ya magonjwa ya akili pamoja na kuboresha viwango vya cholesterol mwilini.
 
CHAI NYEUSI (BLACK TEA)

Wanasayansi wamegundua kwamba wale wanaokunywa vikombe viwili au vitatu vya chai nyeusi kwa siku, wana asilimia 50 ya kubaini mapema dalili za ugonjwa wa akili ikilinganishwa na wasiokunywa kabisa.

Aidha utafiti umebaini kuwa, kunywa chai ya aina hii kunapunguza athari za kupata ugonjwa wa kiharusi, na pia kunalinda mapafu yasidhurike kutokana na uvutaji wa sigara.
 
CHAI YA KAHAWIA (PEPPERMINT TEA)

Utafiti umegundua pia kuwa chai aina ya kahawia inaaminika kusaidia mmeng’enyo wa chakula na kudhibiti msongo wa mawazo.

Viini aina ya menthol vilivyoko kwenye chai aina hii husadia kulainisha misuli, kitu ambacho hatimaye husaidia kupunguza kiwango cha msongo wa mawazo na wasiwasi wanaokuwa nao watu.

CHAI YA OOLONG (OOLONG TEA)

Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha viini aina ya antioxidants, Wanasayansi wanasema kunywa chai aina ya Oolong kupunguza kiwango cha cholesterol mwilini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…