Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kukosa usingizi ni tatizo la kiafya na kwa sababu hiyo ni lazima liangaliwe kwa uzito unaostahili. Wahudumu wa afya hawana budi kuwauliza wagonjwa wao kuhusiana na hali ya kupata usingizi,” anasema Dk Ruth Benca, mtafiti wa masuala ya usingizi wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison nchini Marekani.
 
Kukosa usingizi ni tatizo la kiafya na kwa sababu hiyo ni lazima liangaliwe kwa uzito unaostahili. Wahudumu wa afya hawana budi kuwauliza wagonjwa wao kuhusiana na hali ya kupata usingizi,” anasema Dk Ruth Benca, mtafiti wa masuala ya usingizi wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison nchini Marekani.
 
Ingawa kitaalamu inafahamika kuwa binadamu anahitaji kulala usingizi kwa muda usiopungua saa nane ili awe na afya njema, kutokana na sababu mbalimbali watu wengi wanasumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi.

Takwimu toka vyanzo mbalimbali zinaonyesha kuwa, asilimia 25 ya watu wazima wanasumbuliwa na matatizo ya usingizi na kiasi cha asilimia sita hadi 10 wanasumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi.
 
Kisisitiza kuhusu ukubwa wa tatizo la kukosa usingizi, Dk Rachel E. Salas, Profesa msaidizi wa masuala ya mfumo wa fahamu katika Kitivo cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Johns Hopkins anasema: “Tatizo la kukosa usingizi siyo jambo linalojitokeza wakati wa usiku tu, ni tatizo la ubongo kwa saa 24, sawa na taa ya umeme inayowaka wakati wote, hata wakati wa mchana.”
 
Kukosa usingizi kwa muda mrefu siyo ugonjwa ila ni moja ya dalili ya baadhi ya magonjwa au matatizo ya kiafya. Mtu anaweza kushindwa kupata usingizi unapokwenda kulala (mwanzoni) au kushindwa kupata usingizi tena baada ya kuamuka katikati ya muda wa kulala. Mwanzoni mtu analala vizuri, kisha usingizi unakatika na hapati tena usingizi. Lakini pia kuna baadhi ya watu hupata usingizi lakini wanaamka mapema kuliko kawaida.
 
Wataalamu wa afya kimsingi wanaligawa tatizo la kukosa usingizi katika makundi manne kulingana na muda au urefu wa kipindi cha kukosa usingizi.

Kundi la kwanza ni la kukosa usingizi katika kipindi cha mpito. Katika kundi hili watu hushindwa kupata usingizi kuanzia siku moja hadi kipindi cha juma moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…