Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kundi hili linajumuisha pia nyanya ikiwa ni pamoja na ketchup, tomato sausi, rangi bandia za vyakula na kemikali za kuongeza muda wa matumizi kwenye chakula na viungo kama vile mdalasini, pilipili ya unga na karafuu.
 
Vingine ni vinywaji kama vile chai, pombe, chocolate, cocoa, na jamii ya cola,siki (vinegar) na vyakula vyenye siki kama vile achari na ketchup.

Hisia hizi zinajidhihirisha kwa dalili kama vile maumivu ya kichwa, kuwashwa kwa ngozi, msongo, kiungulia kikali, kubanwa kwa njia ya hewa (nasal congestion), nakadhalika.
 
Histamine ni moja ya kemikali zinazozalishwa na mwili pale kinga za mwili zinapojibu shambulizi au mashambulizi ya kitisho chochote dhidi ya mwili. Histamine hufanya kazi hii kwa kusababisha vimishipa vidogo vya damu kupanuka ili kuwezesha chembechembe nyeupe za damu, pamoja na baadhi ya protini kupita kwa urahisi, kwenda kupambana na kitisho chochote ambacho kimeuvamia mwili.
 
Kemikali hii hufanya pia kazi ya kuratibu baadhi ya shughuli za kifiziolojia zinazoendelea katika njia ya chakula, hasa tumboni. Histamine inafanya pia kazi kama ‘neurotransmitter’ yaani kemikali inayopokea, kukuza na kusafirisha mawimbi ya umeme yaliyobeba taarifa maalumu kutoka katika seli zinazounda mishipa ya fahamu hadi katika seli nyingine katika mwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…