Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutambua hisia kwa wengine. Kipengele kingine cha akili ya kihisia ni kiwango chako cha kutambua hisia za wengine ambacho unacho au ni mwepesi kiasi gani kuhisi hisia za wengine na jinsi gani unajumuika na watu wengine.
 
Utunzaji mahusiano. Hii inahusiana na kiwango chako cha stadi za kijamii. Kuwa na ufanisi zaidi baina ya watu na kuweza kujadili mgogoro na kujenga mtandao wa msaada kijamii, ndivyo unavyozidi kuwa na akili ya kihisia.
 
Bila shaka, watu wana viwango tofauti vya akili ya kihisia na wanaweza kuwa na kiwango cha juu katika Nyanja Fulani kuliko Nyanja nyingine. Watu wenye viwango vya juu vya akili ya kihisia vya ujumla huwa wanapenda kuchukua majukumu ya uongozi, wanajiamini, wana hali ya kudai haki zao, wanaonesha hisia zao moja kwa moja na ipasavyo, wanajisikia vizuri, wanaomaliza muda wao, na hukabiliana vizuri na msongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…