hukimbilia kwenye utumbo mdogo ambako huzaliana. Wakiwa wengi, huenda kwenye utumbo mkubwa na kuanza kushambulia mwili.
Wakikua, huishi katika kinyesi cha binadamu kisha hutolewa kwa njia ya haja kubwa na kuishi katika ardhi kwa muda wa wiki nne, kipindi ambacho huwa na uwezo wa kusababisha maambukizi kwa yeyote atayekutana nao. Wanaweza kusambazwa kwa kutokunawa mikono vizuri baada ya kujisaidia, kusambazwa na nzi, kusafisha vyombo kwa maji yasiyo salama au kushikana mikono na mtu mwenye bakteria hao.