Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kula mlo kamili kwa wakati muafaka na epuka viporo.
iii. Punguza matumizi ya vyakula vyenye asili ya gesi kama maharagwe, njegere n.k
iv. Matunda yenye tindikali nyingi sio mazuri hususani kwa mgonjwa aliyeanza dozi ya vidonda vya tumbo. Mfano wa matunda hayo ni; machungwa, ndimu, Limao n.k
v. Epuka kuwa na msongo wa mawazo kwani wakati mwingine hupunguza uwezo wa mwili kuzuia kiwango cha tindikali mwilini.
 
DALILI ZA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO



Kunaweza kusiwe na dalili za moja kwa moja za ugonjwa wa vidonda vya tumbo lakini mara nyingi ishara zifuatazo zimekuwa zikijitokeza hivyo ni vema kumuona mtaalam wa masuala ya afya kwa ajili ya ushauri wa kitabibu ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vipimo ili kubaini tatizo.
 
Tiba hii inafaa kwa kutibu vidonda vya tumbo vilivyo katika hatua za awali.

Mgonjwa anapaswa kunywa lita moja ya maji masafi na salama alfajiri kabla ya jua kuchomoza na kabla hajakisafisha kinywa chake wala kunawa uso au kupata kifungua kinywa. Kisha mgonjwa anapaswa kusubiri kwa dakika 45 kabla ya kupata chakula cha mchana na asinywe maji yoyote baada ya kula chakula hicho cha mchana kwa dakika 45.
 
Wakati wa usiku mgonjwa anapaswa kunywa maji lita dakika 45 kabla ya kula chakula cha usiku na akae dakika 45 kabla ya kwenda kulala.

Tiba hii huchukua muda wa siku kumi mpaka mwezi mmoja kabla ya kupata nafuu. Katika kipindi hiki chote mgonjwa anapaswa kuzingatia masharti juu ya ulaji na vitu vya kuepukwa.
 
Kunywa juisi ya kabeji mbichi baada ya kuikatakata vipande kisha isage kwenye mashine ya kutengenezea juisi (Blender). Baada ya hapo pima kwenye kikombe kimoja cha chai na unywe mara nne kwa siku. Tiba hii inaweza kutibu tatizo la vidonda vya tumbo kwa muda wa siku kumi. Kumbuka kuzingatia masharti ya msingi yaliyoainishwa hapo juu.
 
Asali ina chembechembe za asili zenye kuua bacteria na virusi ambazo vina uwezo wa kuua helicobacter Pylory ambao ni wadudu wanaosabisha ugonjwa huu kitu kinachomaanisha kuwa ina uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo. Kingine ni kwamba asali huweza kulainisha umio, mfuko wa chakula na utumbo hivyo huweza kufunika vidonda vilivyopo tumboni. Kutokana na kufunika vidonda maumivu ya kuchoma pamoja na dalili nyingine za vidonda vya tumbo hupungua.
 
Asali pia huweza kusafisha uvimbe na kusafisha vidonda ambavyo hujitokeza kwenye njia ya chakula. Asali inayopaswa kutumika kwa kusudio hili inapaswa iwe mbichi na isiwe imeongezewa vitu vingine na dozi yake ni vijiko vya chakula viwili mpaka vitatu kwa siku.
 
Viungo hivi hufahamika kwa kusaidia katika kutibu vidonda vya tumbo hata pale vinapotumika vikiwa vimechanganywa na vyakula vingine kutokana na nguvu nyingi iliyomo ndani yake pamoja na chembechembe zenye kuamsha na kuboresha mwili zilizomo ndani yake ambazo huwezesha kuukinga mwili dhidi ya maambukizi kama vile vidonda vya tumbo.
 
Viungo hivi hufahamika kwa kusaidia katika kutibu vidonda vya tumbo hata pale vinapotumika vikiwa vimechanganywa na vyakula vingine kutokana na nguvu nyingi iliyomo ndani yake pamoja na chembechembe zenye kuamsha na kuboresha mwili zilizomo ndani yake ambazo huwezesha kuukinga mwili dhidi ya maambukizi kama vile vidonda vya tumbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…