TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 24.08.2017
Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumtaka
winga wa Chelsea Willian, 29. (Times)
Chelsea wamepanda dau jipya la pauni milioni 35
kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberl
ain, 24. (Telegraph)
Chelsea wanajiandaa kutoa pauni milioni 32
kumsajili kiungo wa Leicester Danny Drinkwater,
27. (Sun)
Nyota wa Chelsea Eden Hazard atafanya kila
awezalo kulazimisha uhamisho wake kwenda
Real Madrid msimu huu. (Don Balon)
Beki wa kati wa Southampton Virgil van Dijk
amekutana na Chelsea bila ruhusa ya klabu yake.
(Star)
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo,
32, huenda akaondoka Hispania kabla ya mwisho
wa wiki hii. (El Pais)
Kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25,
anafikiria kutoa taarifa rasmi kwa umma
kuzungumzia kutoridhishwa kwake na klabu hiyo,
ili kulazimisha uhamisho wake. (Yahoo Sports)
Juventus wanapanga kupambana na Liverpool
katika kumsajili beki wa Schalke Benedikt
Howedes. (Bild)
Inter Milan wamepanda dau la kumtaka beki wa
Arsenal Shkodran Mustafi, 25, kwa mkopo, katika
mkataba wa kumsajili kikamilifu baadaye kwa
pauni milioni 20. (Mirror)
Baba yake Lionel Messi amezungumza na
Manchester City kuhusiana na mwanae huyo
kuhamia Etihad. (Sun)
Kylian Mbappe, 18, anakaribia kukamilisha
uhamisho wake kwenda PSG kwa euro milioni
150. Monaco na PSG tayari zimefikia
makubaliano ingawa wanasubiri kuona nani kati
ya Julian Draxler, Lucas Moura au Javier Pastore
atakuwa tayari kwenda Monaco kama sehemu ya
mkataba huo. (L’Equipe)
Beki wa West Brom Jonny Evans, 29, anatarajia
kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30
kwenda Manchester City wiki ijayo. (Mirror)
Manchester City hawajakata tamaa ya kumsajili
Alexis Sanchez, 28, na wanafikiria kupanda dau
la pauni milioni 50, kumsajili mchezaji huyo kabla
dirisha la usajili halijafungwa wiki ijayo. (Times)
Manchester City wanataka kupanda dau la euro
milioni 40 kutaka kumsajili beki wa Espanyol
Aaron Martin, 20. (Sport)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho
amezuia uhamisho wa mkopo wa kiungo Andreas
Pereira kwenda Valencia. (Marca)
Barcelona wamekuwa na mazungumzo na PSV
Eindhoven kuhusiana na uhamisho wa winga
kinda Steven Bergwijn, 19. ( gianlucadimarzi
o.com )
Schalke wamewaambia Barcelona wanaweza
kumsajili Leon Goretzka, ili kuzuia mahasimu
wao Bayern Munich wasimchukue. (Mundo
Deportivo)
Vincent Janssen na Kevin Wimmer wa
Tottenham wanakaribia kuhamia West Brom.
(Sun)
Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala
anakaribia kuhamia Inter Milan. (Sky Sports)
Paris Saint-Germain wanafikiria kumsajili kipa wa
Napoli Pepe Reina, 34. (AS)
Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa
Angel Di Maria, 29, kutoka PSG. (Sport)
Tottenham wanajiandaa kupanda dau jipya
kumtaka mshambuliaji wa Lazio Balde Diao, 22,
ambaye pia amehusishwa na kwenda Juventus.
(Corriere dello Sport)
Tottenham wapo kwenye mazungumzo ya kina
na PSG kuhusu uhamisho wa beki Serge Aurier
kwa pauni milioni 24. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell, 25,
ameiambia klabu yake kuwa hataki kwenda
popote kwa mkopo msimu huu. (Guardian)
Arsenal watakubali pauni milioni 14 kutoka kwa
Deportivo La Coruna ili kumsajili Lucas Perez
kabla ya dirisha la usajili kufungwa wiki ijayo.
(Evening Standard)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara
zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya
wachezaji waliokamilisha rasmi usajili b