Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1. Sio sawa sana kumuacha mtoto wa miaka miwili kuangalia TV; hasa kumuwekea chumbani kwake ili eti acheni nk

Huko Marekani tafiti zinaonyesha asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miaka miwili wanaangalia televisheni. Hata hivyo utafiti wa hivi karibuni wa taasisi ijulikanayo kama The American Academy of Pediatrics umeonyesha kuwa kuwapa fursa watoto kuangalia TV na hasa kuwapa muda mrefu kuangalia TV hakuwasaidii
 
chochote zaidi kunawaumiza, watoto ndio kwanza wametoka kuzaliwa, wanatakiwa waachwe wakue akili zao polepole, sio kuanza kuwamezesha vitu visivyo na maana. Mtalaamu wa masuala ya ubongo wa taasisi hiyo Roberta Golinkoff, ambaye ni mwandishi mwenza wa utafiti mwingine Einstein Never Used Flashcards: How Our Children Really Learn—And Why They Need to Play More and Memorize Less.
 
Mtafiti huyo anasema “Lugha ni muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu, na kwamba lugha ambazo wanakutana nazo kwenye televisheni hazina msaada kwao, ni uchafu tu wanaingizwa kwenye ubongo. Mengi ya yale ambayo yanaonekana kwenye televisheni au kama ni vichekesho, havijibu maswali muhimu kuhusu maisha yao ya kila siku huko mbeleni…watu wanahitaji kujifunza vitu vya maana sio vikaragosi au vitu vya vita ama vichekesho”.
 
Kama unataka kuwa na mtoto smart, mwache apumzike wala usimsikilizishe uchafu…anachokisikia mara nyingi au anachokiona mara nyingi ndicho kinachojaa kwenye ubongo wake”
Watafiti wengine, Elizabeth A. Vandewater, et al. “Digital Childhood: Electronic Media and Technology Use Among Infants, Toddlers, and Preschoolers.” Pediatrics, 119 (5), 1006-15, anasisitiza kwamba msingi wa
 
kuwa na mtoto bora ni kuhakikisha unamlea vizuri kwa kumuonyesha vitu vizuri, sio uchafu na video au kumuonyesha vipindi vya televisheni visivyo na maana kwake. Kama unampa mtoto nafasi ya kuangalia vikaragosi/vichekesho maana yake unataka mtoto wako awe na mambo ya vikaragosi na mambo yasiyo na maana.
 
Ni kama shambani unapanda bangi halafu unatarajia kuvuna mpunga. Hufanyi sahihi.
Mtoto anatakiwa kuangaliwa katika uangalifu wa hali ya juu kwa maana ya malezi na hata ulaji wake. Kwa mfano katika saikolojia tunaamini kwamba mtoto ambaye anakumbana na visa au hali Fulani katika maisha yake akiwa na umri wa miaka 1-6 ubongo wake unakuwa ‘stunted’; kwamba
 
ubongo wake unajifunza kufikiri kwamba maisha ndiyo yale aliyoyaona akiwa na umri huo…jambo huko mbele anaweza kubadilika, lakini itegemea zaidi na aina ya watu ambao atakutana nao, kama atakuwa ni mwenye dini au aina nyingine ya ushauri mzito unaoweza kumtoa kwenye hali hiyo.
 
2.Kama huna sababu za maana sio sahihi kumuachishwa mtoto kunyonya haraka; Mtoto mwenye umri wa miaka 6 ambaye amenyonyeshwa vizuri, walio wengi, huwa na uwezo mzuri zaidi kuliko yule ambaye hakunyonyeshwa vizuri, hii ni katika testi za kuangalia uwezo wa ubongo (IQ tests).
 
Hili ambalo nalizungumzia juu, limethibitishwa na tafiti mbalimbali, ikiwamo ya raia wa Belarusi na watoto wao; kwamba kulikuwa na makundi mawili, ya kinana ambao walikuwa wakiwanyonyesha watoto wao mara kwa mara bila kuwapa kitu kingine zaidi kwa mwaka mzima. Kundi la pili katika utafiti huo ni la wanawake ambao hao ni wale akina bizeeeeee…bizeeee bizeeee unaijua bizeee wewe….hao ni wale
 
ambao waliwanyonyesha watoto kwa shida, kwamba ndani ya miezi kadhaa hadi mwaka watoto wamekuwa wakipambana na vyakula vingine vya ajabu kama uji na kadhalika huku wakati mwingine wakinyonya kidogo kuliko wanavyokula vitu vingine (kwamba ukijumlisha vitu ambavyo vinaingia tumboni mwa mtoto kwa siku, unakuta uji, maji ya kuchemsha sijui ya dukani na kadhalika ni mengi zaidi hayo
 
kuliko maziwa halisi ya mama); Utafiti ulikuja na matokeo kwamba wale watoto ambao wazazi wao waliwanyonyesha mwaka mzima bila kula kitu kingine zaidi ya maziwa ya mama zao (hata kama ni maji nk basi yalikuwa kidogo kuliko maziwa ya mama zao), hao walikuwa na uwezo mkubwa sana katika kusoma, kuandika na hesabu. Naomba nieleweke kwamba hapa sizungumzii maziwa ya makopo, hayo ni sawa na uji nk..nazungumzia mtoto kunywa maziwa halisi ya mama yake, sio vitu vingine.
 
Jambo la msingi sana kwa mama kumpata mtoto ambaye atakuwa smart kichwani ni kuhakikisha anamnyonyesha vizuri; kwamba kipaumbele chake kinakuwa ni kuhakikisha mwanae ananyonya zaidi na tumbo la mtoto kuwa na maziwa mengi zaidi ya mama yake mzazi, badala ya vitu vingine.
Haya sio tu maneno ya Dismas Lyassa, bali hata wasomi wengine wanakiri hilo kwamba kunyonyesha ni jambo muhimu sana kwa ukuaji wa mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…