Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Teknolojia ya Li-Fi iligunduliwa mwaka 2011 na mwanazuoni aitwaye Prof. Harald Hass ambaye aliizungumzia teknolojia ya Li-Fi katika onyesho linajulikana kama TED Talk na hatimaye mwaka 2012 teknolojia ya Li-Fi ilizinduliwa rasmi.
 
Li-Fi ni nini?

Li-Fi (Light Fidelity) ni teknolojia mpya na ya kisasa zaidi inayotumia mwanga wa taa (LED Lights) kusafirisha mawimbi na hatimaye kuweza kupata huduma ya intaneti. Teknolojia hii ni tofauti na ile ya Wi-Fi ambayo inasafirisha data kwa kutumia mawimbi ya redio kuweza kupata intaneti.
 
Faida za kutumia teknolojia ya Li-Fi.

Li-Fi inasafirisha kiasi kikubwa cha data ndani ya muda mfupi sana ambapo ni mara 50 zaidi ya uwezo wa teknolojia ya Wi-Fi.
Teknolojia ya Li-Fi haipiti kwenye ukuta hivyo kufanya mtumiaji kutokuwa na hofu ya mtu mwingine ambaye yupo mbali na sehemu alipo kipata huduma huduma ya intaneti kutoka kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…