Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Toleo jipya la WhatsApp laanza kupatikana. WhatsApp imetangaza kufanya maboresho ya programu yake pendwa kwa kuweka kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtumiaji wake kutumia aina ya Fonts(herufi) mbalimbali azitakazo.
 
Kipengele hicho kipya kitakuwa katika sehemu ya kuweka Status ambapo mtumiaji ataweza kuweka background ya rangi yoyote aipendayo na kisha kuandika chochote akipendacho kwa aina ya muandiko aupendao.
 
Aina ya herufi za namna tano kwa sasa ndio pekee zinazopatikana pamoja na rangi 22.

Kwa mujibu wa WhatsApp maboresho haya yanapatikana kwa matoleo yote ya Android na iOS. Ili kupata mabadiliko hayo ni lazima ufanye Update kwa WhatsApp yako.
 
Pia kwa wale wanaotumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) kwa sasa wataweza badilisha Status moja kwa moja.

Kumbuka kila baada ya masaa 24 Status itajiondoa na hivyo kulazimika kuiweka tena au kuweka mpya.
 
Kuna zaidi ya App milioni 2 katika soko la Goolge Play kwa wale watumiaji wa Android. Baadhi ya watu huwa wanapata shida katika swala zima la kuchagua ni App zipi bora kuliko zingine.
 
Moja kati ya App za kuwa nazo ni Pocket, hilo halina ubishi (haaha)!. Pocket kazi yake kubwa ni kuwa kama mfuko wako ambao utaweka kila kitu ambacho unataka kukisoma/kukitazama baadae. Kwa mfano kama unakaribia ingia katika mkutano na ukaona makala katika mtandao wako wa TeknoKona unaweza hifadhi makala hiyo katika App ya Pocket alaf baadae ukaja kuipitia.
 
Kumbuka kila siku huwa unaingia katika mtandao ili kupata habari na taarifa zingine inaweza ikawa kifaa chako kikawa na chaji ndogo, App kama hii ndio inakuja kuwa msaada mkubwa kwako. Ukiachana na hili kuna faida nyingi sana za kuwa na App hii. Ili kuipata kwenye Simu ya Android ingia hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…