Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unashangaa kwa nini hufanikiwi?✔
Sikia haihitaji ukalishwe chini ndo uelewe, Ukweli ni kwamba unajishughulisha Sana na mambo yasiyo Kuhusu katika mafanikio.wazungu husema mind your own business sasa Sijui huu msemo unauchukuliaje?? Imagine unamjua Ali kiba hadi bafuni kwake, tour zote za mwaka huu unazijua hadi nyingine unataka kumpangia, nikuulize wewe ni mwanamziki??
 
Umeona eee Uko bize kujua simba na yanga mara mbeya city……. Hivi unataka kuwekeza kwenye soka?? Cha ajabu wewe ni mwalimu tena wa Bible knowledge halafu Uko bize na simba mara yanga. Uko kwenye biashara lakini unafatilia Lini bunge litakua live sijui unataka utangaze biashara yako bungeni . Mara Lema ataachiwa Lini, wewe ni mwanasiasa?? See hauko serious kufatilia biashara yako ya vitunguu ina Changamoto zipi, faida, lugha gani utumie kwa wateja au msimu wa soko ni Lini??
 
Mimi sijawahi kumuona Dewji ana comment kwenye page ya east Africa TV kuchangia Mada zisizohusiana na biashara zake. Unajua matajiri wako bize kufatilia yanayo wafanya kutajirika zaidi wewe Je?? Masikini unafatilia mambo ya kimasikini siyataji unayajua…….
 
Sijui kama utafanikiwa kwa kujua Lady Jay dee siku hizi anaishi wapi Wakati vitunguu vyako viko gengeni, Sijui ghalani Iringa vinaliwa na wadudu na hujui namna ya kuteka soko. Kutwa unamaliza hizo bando za mega mix za tigo kufatilia ubuyu wa sudy brown….. Hahahaha mara unajiita shilawadu…..
 
Utaishia kusoma story za mafanikio ya akina Mengi, Dewji, Dangote, shigongo lakini yako itakua tu HISTORIA YA MAREHEMU KWA UFUPI ulisoma darasa la kwanza hadi Saba shule ya msingi mwembengoma……
Historia inafutika hapo hapo….

RECONSIDER YOUR LIFE,
Mind you own business,
 
Ugumu wa maisha huanzia akilini mwako✔
UGUMU WA MAISHA HUANZIA AKILINI MWAKO.

Ebu fikiria Dada anayechoma mahindi maeneo ya Manzese Darajani kuanzia saa 12 jioni mpaka SAA 2 usiku, kwa siku moja anauwezo wa kuchoma mahindi .50. Kila hindi moja ananunua shambani kwa shilingi 100/- Na Anauza kwa sh.600/-

Hiyo ina maana mahindi 50 ananunua kwa shilingi 5000/- akichoma na kuuza anapata sh.30,000/-. Akitoa pesa ya mtaji (5000/- ya mahindi na 1500/- ya mkaa) anabakiwa na sh.23,500/- kwa siku.
 
Hivyo kwa mwezi huyu mchoma mahindi atakuwa ameingiza kiasi cha sh.705,000/-

Mwalimu mwenye Degree anayeanza kazi analipwa 584,000/- akikatwa kodi pamoja na makato mengene ya mifuko ya jamii anabakiwa na sh.425,000/.

Tofauti ya Mwalimu wa degree na Muuza mahindi ni kuwa Mwalimu kaajiriwa, muuza mahindi kajiajiri. Mwalimu anafanya kazi masaa 9 kwa siku, muuza mahindi anafanya kazi masaa matatu kwa siku (saa 12 jioni hadi 2 usiku).
 
Mwalimu anatumia muda wake wa ziada kusahihisha mitihani na homework, mchoma mahindi anatumia muda wake wa ziada kutafuta fursa nyingine za kupata hela.

Uoga wako ndio umaskini wako.
KAMA HUNA FURAHA NA UNACHOKIFANYA BADILI MTAZAMO NA SIKUSHAURI UKAUZE MAHINDI NO HUO NI MF. KAMA SWALA NI KIPATO TU BASI KUNA FURSA NYINGI SANA KIPINDI HIKI NA WAWEZA BILA HATA YA KUWA NA MTAJI CHA MSINGI NI WEWE KUAMUA KUWAONA WATAALAMU WAKUSHAURI NI NINI CHA KUFANYA.
 
Umenena jambo zito sana ,yaan hilo ndo tatzo twashindwa litambua vijana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha boss na mwajiri wake✔
BARUA YA BOSI ILIBADILI FIKRA ZANGU KUHUSU PESA KATIKA DAKIKA ZA MWISHO ZA MAISHA YANGU
Duna Lawrence (78) ni raia wa Togo ambaye alijitosa kwenda nchini Ujerumani kutafuta maisha mwanzoni mwa miaka ya 80. Baada ya kufika huko, alipata kazi, akawa muaminifu kwa Bosi wake ili aweze kupata mafanikio.

Baada ya miaka mingi kupita, Duna alirudi nchini mwake kwa mara ya kwanza na akaoa, kisha kurejea tena Ujerumani. Bwana Duna aliendelea kufanya kazi kwa bidii huku mafanikio yake kimaisha yakizidi
kushuka chini, akaomba kuongezewa mshahara ili kukidhi mahitaji yake, lakini hiyo haikumpa unafuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…