Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Namna ya kufanya

“Kuhakikisha kuwa joto lako la mwili linashuka vizuri, badala ya kuvaa soksi unapolala weka miguuni dumu la maji ya moto,” anasema Dk Idzikowski.

“Soksi haziruhusu joto kupungua miguuni, badala yake utaishia tu kuungua. Chupa ya maji ya moto inafanya miguu yako kuwa ya moto, lakini itapoa au unaweza kuondoa,” anasema.
 
Kisukari

Kwa mujibu wa utafiti kuhusu kisukari uliofanyika Marekani, wataalamu waligundua kuwa mtu akilala kwenye chumba chenye baridi anaweza kuongeza mafuta (brown fat) kwa watu wazima.

Vijana watano wenye afya nzuri walilala kwenye chumba chenye joto maalumu kwa miezi minne. Mwezi wa kwanza chumba kilikuwa na joto la nyuzi 24, baadaye lilishushwa hadi nyuzi 19, kisha likapandishwa hadi nyuzi 24 na mwezi wa mwisho ilipandishwa hadi nyuzi 27.
 
Vijana hao walikuwa wakila viwango sawa vya kalori na kuangalia namna insulini inavyofanya, kiasi gani kinahitajika ili kiwango cha sukari mwilini kiwe sawa, vyote vilikuwa vinapimwa kila siku.

Matokeo yalikuwa ya kushangaza. Baada ya wiki nne za kulala kwenye chumba chenye nyuzi joto 19, vijana hao walikuwa wameongeza mara mbili kiwango
 
chao cha mafuta ya kahawia mwilini. Matokeo yalionyesha kuwa waliunguza kalori nyingi zaidi mchana wakati chumba chao cha kulala kilikuwa na baridi kali (ingawa si kiasi cha kupunguza uzito) na utendaji wa insulini nao uliimarika.

Mwandishi mkuu wa ripoti hiyo, Francesco Celi anasema kuwa utafiti umebainisha kuwa kutumia muda mrefu kulala kwenye chumba cha baridi kuwaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.
 
Profesa wa maendeleo ya saikolojia katika Chuo Kikuu cha Nattingham na mtaalamu wa mafuta ya kahawia, Michael Symonds, anasema kulala bila nguo kuna faida kubwa.

”Mafuta ya kahawia yanaweza kuzalisha joto mwilini mara 300 kuliko kuliko kiungo kingine chochote mwilini, inamaanisha kama ukiacha iendelee hivyo kwa muda mrefu ungeweza kupunguza nguvu ya ziada,” alisema.
 
Aliongeza: “Kwa hiyo chochote unachoweza kufanya kuchochea, kama vile kupunguza ‘thermostat’ na kulala kwenye baridi, linaweza kuwa jambo la faida sana.”

Hata hivyo, mtaalamu huyo anaonya kuwa joto kwenye chumba lisiwe chini ya kiwango ambalo hutajisikia huru, vinginevyo utashindwa kulala.

Anaendelea kusema kuwa watu wanaosikia joto kali usiku na wanapenda kulala bila nguo, wanaweza kuwa na kiwango kikubwa cha mafuta ya kahawia, ambayo yanasababisha mtu ajisikie joto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…