Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger Ijumaa alisema wachezaji wanahitaji "uwazi" kuhusu hali yao.
Meneja wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson pia alisema soko linafaa kufungwa mapema alipoulizwa kuhusu juhudi za Barcelona kumtaka nyota wa Liverpool Philippe Coutinho.
 
Hali kwamba soko litafungwa mapema ina maana kwamba klabu zitatakiwa kuharakisha kuwanunua wachezaji baada ya Kombe la Dunia la 2018
Msimu wa 2018-19 utaanza baada ya Kombe la Dunia ambalo litafikia kikomo tarehe 15 Julai nchini Urusi.
 
Alexis Sanchez hatatizika kurejea kucheza vyema katika Arsenal baada ya kutoridhika wakati wa kipindi cha kuhama wachezaji kilichomalizika wiki iliyopita, meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger amesema.
Sanchez, 28, alikaribia sana kuhamia Manchester City dakika za mwisho, lakini Wenger amesema "hana shaka kuhusu fikira na msimamo wa Alexis".
 
 
Arsenal walikuwa wamekubaliana uhamisho wake wa £60m na City lakini ilitegemea iwapo wangefanikiwa kumpata Thomas Lemar, ambaye aliamua kusalia Monaco.
"Atarejea upesi sana kucheza katika kiwango chake kizuri kabisa," amesema Mfaransa huyo.
 
"Soko limefungwa kwa sasa, kulikuwa na mambo mengi sana yaliyokuwa yanaendelea. Ni vigumu sana kuzungumza kuhusu hilo kwa sababu Lemar sasa yuko Monaco na lazima aangazie kucheza huko, Sanchez yuko hapa na anaangazia hapa," Wenger ameongeza.
 
Mambo mengi hufanyika sekunde za mwisho ambayo huwa nayajutia. Hii ndiyo maana ninaamini kwamba wakati umefika tubadilishe sheria na tuwe tukifunga soko kabla ya msimu kuanza.
"Wachezaji hawajui hatima yao. Wako ndani au nje? Kuna wengine ambao wanachukuliwa na watu alasiri ya mechi, watu wanaotaka kuwachukua.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…