Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kujenga kasumba ya kutumia pombe (Utumwa wa matumizi ya pombe)
Vidonda vya tumbo
Kuongezeka kwa uzito-Kutokana na kiwango cha wanga katika pombe
Ugonjwa wa mifupa(Osteoporosis)-Pombe inapunguza uwezo wa kalsium kutumika kujenga mifupa
Matatizo ya Uzazi-Wanaume wanapungukiwa nguvu za kiume na wanawake kushindwa kushika mimba kirahisi.
Kunywa pombe kidogo kunaweza kupunguza kwa mkiasi kikubwa madhara haya
 
Gharama za Magonjwa yatokanayo na Pombe:

Gharama nyingine ni zile za matibabu yamagonjwa au madhara yanatokanayo na pombe

Kama ilivyoonyeshwa awali pombe huchangia magonjwa ya moyo,kisukari,vidonda vya tumbo na saratani. Pia huchangia kuumia katika ajali, na uharibifu wa magari na vyombo vingine.

Matibabu ya magonjwa na madhara mengine yaliyotajwa yanaongeza gharama kubwa kwa familia na mtu momoja mmoja.
 
Utendaji na Uzalishaji Hafifu

Ulevi uanapunguza nguvu kazi. Wafanyakazi walevi hufanya kazi kwa ufanisi wa chini kuliko kama wangekuwa wanywi pombe. Huenda kazini wakiwa na pombe kichwani na uwezo wa kufikiri na ufanisi huwa chini katika hali hii.

Baadhi huchelewa kazini au kutohudhuria kabisa kwa baadhi ya siku au hata kwa muda mrefu.
 
3. Madhara ya Unywaji wa Pombe Kijamii


Madhara ya Unywaji wa pombe yako wazi kabisa katika jamii. Majumbani,sehemu za kazi na hata mitaani. Madhara haya ni kama ifuatavyo

Ukosefu wa staha na maadili– Katika ulevi watu wanakosa kujiheshimu, mfano matumizi ya lugha za matusi,ugomvi na hata kujisaidia hadharani ni vitu vinavyotokea.
 
Ubakaji na Ukatili– Katika hali ya ulevi matukio ya ubakaji na ukatili yamelipotiwa majumbani na mitaani
Kuvunjika kwa Mahusiano na Familia- Familia nyingi zinavunjika kutokana na ulevi wa wenza wote au mmojawapo
Kushuka kwa Heshima: Heshima toka kwa jamii inayokuzunguka toka katika familia yako hadi nje itashuka kutokana na mambo unayoyafanya ukiwa umelewa.
 
Kwa kuona madhara yaliyotajwa,kuna kila sababu ya kuacha kabisa kunywa pombe au kunywa kwa kiasi kidogo ili kupunguza madhara yake. Lakini kuishi bila kunywa pombe inawezekana na watu wengi siku hizi wameona hili na wameamua kuishi katika mtindo mpya wa maisha bila pombe.
 
Kukosa Muda na Familia: Walevi wanatumia muda mwingi katika unywaji na hivyo kuwa na muda kidogo na familia zao na hivyo kukosa mshikamano na wenza wao na watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…