Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HIVI NDIVYO SAID SALIM AWADH BAKHRESA ALIVYOTOKA KWENYE UMASKINI MPAKA KUWA BILIONEA.

Said Salim Awadh Bakhresa alizaliwa mwaka 1949 mjini Zanzibar, alisoma elimu ya msingi hadi alipofikia umri wa miaka 14 ambapo aliacha shule kutokana na maisha ya familia kuwa magumu hivyo kujiingiza katika biashara ili aweze kuhudumia familia katika mahitaji kama chakula baada ya baba yake kukabiliwa na madeni.

Katika miaka ya 1960, wakati Tanzania ilipokuwa nchi ya kijamaa na Kenya ikifuata siasa za kibepari, Bakhresa aliweza kununua mabaki ya mazao ya baharini kama, mifupa na magamba ya viumbe wa baharini na kuyauza Mombasa.

Kutokana na tofauti ya kifedha iliyokuwapo wakati huo, aliweza kununua ngozi za viatu kutoka Kenya na kuzitumia kushonea viatu hapa Tanzania.
Badae alifanya kufanya biashara ya viazi, mikate na ice cream.

Katika miaka ya 1970 Bakhresa alifungua na kuendesha biashara ya mgahawa.
Mgahawa huu alinunua kutoka kwa mgeni wa kihindi ukiwa na jina la AZAM,jina ambalo analitumia kama nembo(brand) ya bidhaa zake kwa sasa.

Katika miaka ya 1990 alinza uwekezaji katika viwanda. Kwa sasa kiasi kikubwa cha mchele na bidhaa za nafaka zinatoka katika kampuni ya Bakhresa Group iliyopo kipawa (flour Mill).
Nchi jirani ya Rwanda kwa mfano, inategemea tani 120,000 za unga wa wangano kwa mwaka kutoka kwa kampuni ya Bakhresa.

Said Salim Awadh Bakhresa ni Mwenykiti wa makampuni ya Bakhresa Group, ni Mtanzania anayemilki viwanda vingi vinavyozalisha bidhaa za vyakula zinazouzika ndani na nje ya
nchi.

Pia kokote jijini Dar-es- salaam na mikoani, bidhaa za AZAM utasikia zikitajwa. Azam ni nembo(brand) ya bidhaa zinazotengenezwa kupitia makampuni ya Bakhresa, Azam ni neno la kihindi linalomaananisha ukubwa.

Bakhresa amejijengea jina kibiashara kwani si ajabu kusikia watu wakisema, Amka na Azam, shinda na Azam au sheherekea na Azam.
Tafsiri yake ni kwamba katika maisha yetu ya kila siku, tunatumia bidhaa za Azam kwa kiasi kikubwa sana.

Mapato yake kwa mwaka ni zaidi ya dola za Kimarekani $520 milioni (zaidi ya Tshs Trilioni 1) huku akiwa ana wafanyakazi zaidi ya 2,000 wenye ajira rasmi.

Bakhresa ni mtu mashuhuri katika harakati za mapinduzi na maendeleo ya viwanda Tanzania Bara na Visiwani.

Katika muda wa miongo mitatu tu ameweza kujenga timu imara ambayo inasimamiwa na wakurugenzi makini ambao ni watoto wake mwenyewe.
Bakhresa Group ina matawi katika nchi sita ambazo ni Rwanda, Burundi, Uganda, Malawi, Zambia na Msumbiji.

Amejikita zaidi katika usindikaji wa vyakula. Ana viwanda vya kusaga unga wa ngano na mahindi, viwanda vya ukoboaji wa mchele, uandaaji wa vyakula kama mikate,chapatti, vinywaji
kama maji (Uhai) , juisi za matunda na soda, pamoja na ice cream.

Pia ana kiwanda cha vifungashio vya bidhaa mbalimbali, biashara ya mafuta ya magari na mitambo.
Vilevile anazo boti za usafilishaji abiria ambazo hufanya safari zake katika Bahari ya Hindi.
Hali kadhalika, anafanya biashara ya usafirishaji mizigo (azam logistics).

Katika michezo ,Bakhresa anamiliki timu ya mpira wa miguu ijulikanayo kwa jina la Azam Footbal Club ambayo imefikia kiwango cha kucheza ligi kuu Tanzania bara.

Unapomzungumzia Said Salim Bakhresa unamzungumzia mtu
anayesimamia maono yake na kuhakikisha yanatimilika kikamilifu.

Ana uzoefu mkubwa katika usimamizi wa biashara , ni mtu anaye fanya tafiti juu ya maendeleo ya viwanda na masoko katika kutambua mahitaji ya watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Licha ya kutangaza bidhaa zake kupitia redio na televisheni, anapata fursa ya kujitangaza kupitia timu yake ya mpira wa miguu anayoimiliki(Azam Football Club) hivyo anatangaza bidhaa zake kupitia michezo.
Vilevile anawatumia wachuuzi au Machinga katika kutangaza bidhaa zake mfano Ice cream.

Pamoja na mafanikio makubwa aliyonayo bado kuna vikwazo na changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo ili kufikia malengo yake.
Kwa mfano sera za biashara zisizo simamiwa vizuri katika ushindani wa masoko, gharama za teknolojia katika uzalishaji n.k.

Bakhresa ni mtu anayehamasisha Watanzania wasiogope kujifunza kwa vitendo, kwani wengi huhofia changamoto zinazoweza kusababisha, anguko katika biashara lakini mjasiliamali anapaswa kujiamini katika mawazo yake na kujiwekea mipango mathubuti.

Kwa sasa bado Bakhresa anaendelea kutanua wigo wa biashara katika kuweza kufikia nchi nyingi zaidi duniani.
Hata hivyo anaamini kwamba bidhaa zake bado hazijatosheleza soko la ndani .

Pia anatoa ushauri kwa Watanzania, hususani vijana, wajitahidi kufikili vizuri na kutazama fursa zilizopo nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itawainua wao kiuchumi, ili hatimaye kuondokana na umaskini unaolikabili taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…