Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI?



Ushauri wa pekee ni kukimbia tu, kwani hakuna namna yoyote inayoweza kukufanya utoke salama, mnyama huyu ana nguvu kubwa ya mwili na ni kiumbe ambaye huwezi pambana naye hata ukiwa na silaha kwa sababu ya ngozi yake ngumu.
 
Epuka kukaa sehemu ambazo kuna uwezekano wa uwapo wa kiumbe huyu ni hatari, sehemu hizo ni kama mito iliyopo vijijini au mbugani, kaa mbali kabisa na fukwe za maziwa na wala usidiriki kunawa au kutaka kunywa maji yake pasina ruhusa ya anayewaongoza.
 
FAHAMU HATARI YA FISI NA MAMBA Wanyama hawa pamoja ya kuwa na sifa nyingi zinazofanana, kama kuwinda, kutumia nyama kama chakula kikuu, lakini yakupasa ujue ni wanyama wenye mfumo hatari sana wa meno, katika hili ili unielewe vyema fanya zoezi dogo lifuatalo, meno yako ya juu yakutanishe na ya chini ! kama umefanya hivyo ni wazi umebaini ya kwamba meno yako yanapokutana ya juu yanabaki kuwa ya juu na ya chini yanabaki kuwa ya chini,
 
Mfumo wa meno ya aina hiyo unapouma (ng'ata) huwa unapelekea nyama kukatika, lakini pia mfumo wa aina hiyo hiyo upo wa aina nyingine ambao huwa na meno kadhaa yaliyochongoka sana na marefu hasa ya pembeni kama ilivyo kwa wanyama jamii ya paka yaani mbwa, simba, chui nk hawa wanapouma hunyofoa nyama. Tofauti na wanyama wengine meno ya fisi na Mamba yanapokutana hupishana,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…