Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MFAHAMU MBUNI Mbuni ndiye ndege mkubwa kuliko ndege wote waishio juu ya uso wa dunia, ndege huyu ana sifa ya kuwa na miguu mirefu sambamba na shingo ndefu zaidi, jambo linalomfanya awe na muonekano wa urefu sana, ana macho mawili yenye ukubwa sana ambayo humuwezesha vyema kuona umbali mrefu, mdomo wake huwa na ufanano na mdomo wa bata na juu ya mdomo wake kuna matundu mawili ambayo ndio sehemu ya pua,
 
viumbe hawa hutofautiana rangi kutokana na jinsia zao, dume huwa mweusi na jike huwa na rangi nzuri na ya kuvutia ya kahawia. Pamoja na sifa zote hizo nzuri kwa bahati mbaya mbuni hajui kupeperuka, ni ndege anayetumia miguu tuu kukimbia, huwa na urefu futi 7 mpaka 9, huku uzito wao ukiwa zaidi ya kilo 140, ndege hawa huishi miaka mingi ni zaidi ya 40, pia ndege huyu ana uwezo wa kukimbia kilometa 50 kwa saa, kwakuwa huanza mbio zake taratibu na baadaye kuchanganya zaidi kadri akimbiavyo,
 
mwili wake ukiwa umejichochea na ukaanza kumuhesabu akiwa katika kasi hiyo ya mwili wake unapokuwa mwepesi basi huweza kukimbia kilometa 70 kwa saa. Marafiki wakubwa wa kiumbe huyu ni wanyama wanaokula majani tuu, hasa wale wapole kama twiga, pundamilia,paa nk, lakini upande wa maadui zake ni pamoja na wanyama wote wanaokula nyama, ukiondoa hao mbuni humchukia sana fisi na nyani kwakuwa wanatabia ya kuiba mayai yake, mayai yake huwa ni makubwa na yana uzito wa kilo moja na nusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…