Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

TATIZO LA KUKOSA CHOO
Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.
Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku,lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.
Tatizo la kukosa choo ( Constipation ) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.
Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula vya fiba(Vyakula vyeneye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha zoezi la usagaji wa chakula tumboni.
 
Baadhi ya Vitu vinavyosababisha Tatizo la Kukosa Choo:
Kutokunywa Maji ya Kutosha
Kutokula vyakula vyenye fiba kama matunda na mboga za majani
Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi
Unywaji wa maziwa kupita kiasi
Kutofanya kaziza kushughulisha mwili na kukosa mazoezi
 
Vyakula Vinavyosaidia Kutibu Tatizo la Kukusa Choo
1. Tende
Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitol– aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.
 
2. Maji
Kunywa maji kwa wing kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanahochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini. Fiba zinahitaji maji ili kufanya kazi ya kufagia uchafu tumboni na maji yanapokosekana hunyonya toka katika uchafu tumboni na kufanya choo kuwa kikavu na kusababisha ugumu wa kutoka.
Wataaramu wa afya wanashauri kunywa galsi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)
Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.
 
3. Kahawa na Vinywaji Vingine vya Moto
Kahawa na vinyaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.
Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo
 
4. Ulaji wa Matunda au Saladi
Matunda yanasaidi kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.
Pia ulaji wa matunda ni muhimu kuzingatia muda wa kula, ni vyema kula matunda saa moja au dakika 30 kabla au baada ya chakula. Kula matunda mara baada ya kula kama wengi wanavyofanya ni makosa na kunakukosesha faida zinazotarajiwa.
 
Ulaji wa Mboga za Majani
Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.
Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.
Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.
 
Mambo 8 ya Kuharakisha Kuunga kwa Mifupa Iliyovunjika

Watu kwa mamia huvunjika miguu kote duniani kila siku kutokana na ajali mbalimbali hasa zinazohusisha usafiri kama magari na pikipiki. Wengine huvunjika wakiwa kazini na hata majumbani. Wote hawa wanahitaji kuunganishwa mifupa yao ili wapone na kuendelea na maisha.
Kuunga kwa mifupa iliyovunjika huchukua muda mrefu na hivyo kuwafanya watu waugue kwa kipindi kirefu na kushindwa kuendelea na kazi zao. Lakini kuna mbinu za kusaidia kuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika ambazo zikifuatwa zitasaidia watu kupona kwa haraka.
Kwa ujumla uungaji wa mifupa inategemea sana umri wa mgonjwa na ulaji wake wa chakula chenye virutubisho muhimu. Mchanganyiko sahihi wa madini,vitamini na protini ni jambo la msingi kuzingatiwa.
 
Mambo 8 Muhimu Kuharakisha Kuunga kwa Mifupa Ilivyovunjika
1. Madini ya Kalisiam ( Calcium )
Kalsiam inachukua asilimia kubwa katika mfupa na ni madini muhimu sana katika kuunga kwa mifupa iliyovunjika. Kalsiam inapatikana katika vyakula lakini mgonjwa anaweza kutumia vidonge vyenye Kalsiam.
Ila ifahamike madini haya pekee hayatoshi,ni lazima kuwepo na vitu vingine kama vinavyoelezwa hapa chini
Vyakula Vyenye Kalsiam Kwa Wingi:
Mziwa na mtindi
Soya
Mboga za majani
 
2. Vitamini Muhimu toka Katika Mlo Kamili
Mlo kamili wenye mchanganyiko wa vitamini,madini na virutubisho vingine muhimu katika mwili wa binadamu ni muhimu sana kwa mgonjwa aliyevunjika mifupa.
Vitamini D ,C na K zinahitajika kwa wingi kuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika.
Vitamini D:
Upungufu wa vitamini hii inafanya kalsiam isifike sehemu inayohitajika toka katika damu.
Vitamini D inasaidia kunyonywa kwa kalsiam toka katika damu na kuelekezwa katika mifupa iliyovunjika ili kusaidia uungaji.
Vyakula Vyenye Vitamini D kwa Wingi:
Samaki au mafuta ya samaki
Kiini cha mayai
Bidhaa za maziwa
 
Vitamini K:
Vitamini K inasaidia kuimarisha protini aina ya
osteocalcin ambayo ni sehemu ya muundo wa mfupa. Vitamini K huifanya protini hii kuwa nzito na ngumu na hivyo kusaidia kuimarisha mfupa unaoounga.
Vyakula Vyenye Vitamini K kwa Wingi:
Mboga za majani
kauliflawa
Samaki
Mayai
 
Vitamini C:
Vitamini C inasaidia kupona kwa mifupa iliyovunjika. Vitamini C kama inavyosaidia kupona kwa vidonda inasaidia pia kuunga kwa mifupa kwa kusaidia kuundwa kwa chembe za kolageni ( collagen ) ambazo zinatengeneza mifupa.
Vyakula Vyenye Vitamini C kwa Wingi:
Machungwa na Ndimu
Kabichi na Mboga za kijani
 
Kupunguza Matumizi ya Dawa za Maumivu
Dawa za kupunguza maumivu ni muhimu kwa mgonjwa aliyevunjika mifupa, kwani anakuwa kwatika maumivu makali hasa siku za mwanzo lakini dawa hizi pia zinasababisha kuchelewa kwa uungaji wa mifupa hivyo mgonjwa anashauriwa kutotumia kwa muda mrefu.
 
4. Kuacha Uvutaji wa Sigara
Uvutaji wa sigara unachelewesha kupona kwa mifupa iliyovunjika. Wavutaji wa sigara wanashauriwa kusimama uvutaji wakiwa wagonjwa. Hii inachangiwa na sumu katika sigara kama benzini na karboni dioxide ambazo zinaingilia na kuharibu chembe za mfupa unaounga.
Lakini pia ni kwakuwa sigara inapunguza mzunguko wa damu mwilini kwa kufanya damu kuganda
 
Ulaji wa Protini kwa Wingi
Mfupa unajengwa na protini hivyo inahitajika kwa wingi ili kujenga mfupa imara.

Kufanya Mazoezi
Ili mifupa iunge kwa urahisi na haraka inahitaji mzunguko mzuri wa damu mwilini.
Kwa mgonjwa aliyevunjika hasa miguu huenda hili lisiwe jambo rahisi,lakini mazoezi yanaweza yakahusisha viungo ambavyo havijapata madhara ili mradi visaidie kufanya damu izunguke vizuri.
Mgonjwa anaweza kutembea hata kama anatumia magongo,au kufanya mazoezi akiwa amekaa ili mradi mzunguko wa damu uongezeke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…