Kuna dawa nzuri kabisa zipo ambazo ni mahususi kwa ajili ya kupunguza uzalishwaji wa asidi hiyo au kupunguza asidi ambayo tayari imeshazalishwa. Mifano ya dawa hizo ni Magnesiamu, Omeprazole, Lansoprazole, Cimetidine, Esomeprazole nk
Onyo : Dawa za hapo juu zimeorodheshwa kama mifano tu kwa ajili ya kuelewesha vizuri somo hili. Usiende moja kwa moja kununua dawa yoyote bila kupata ushauri wa daktari. Muone daktari kwanza na ununue dawa baada ya kuandikiwa tu
Punguza uzito wako kama ni mkubwa na epuka kabisa kunywa pombe na kuvuta sigara.