Tengeneza miundombinu ya pesa kukufikia na hiyo miundombinu iko kwenye ndoto zako ,maono yako,kipaji chako na uwezo ulionao.
Kwenye ndoto zako Kuna ramani na barabara za watu kupita kukuletea fedha kutokana na kile ulichonacho,kile ulichonacho ni cha thamani sana.
Kile ulichonacho ni kikubwa zaidi ya fedha ,tafuta kukitimiza hicho ulichonacho ,anza sasa uwezo unao nguvu unayo.
Katika kutimiza ndoto zako usikubali kuzuiwa na fedha,mazingira ,mtazamo hasi,marafiki,jaribu kuwa mtu asiyezuilika ili uweze kuzifikia ndoto zako.